MFUNGAJI wa bao pekee la Simba katika ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS ...
MFUNGAJI wa bao pekee la Simba katika
ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza
hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika
dhidi ya AS Viya, Mkongomani, Chris Mugalu,
ameibuka na kutamba kuwa lazima kitaeleweka
msimu huu katika michuano hiyo
inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika
(CAF).
Mkongomani huyo bao lake la penalti dakika ya
60, lilitosha kuipa ushindi Simba ugenini katika
mchezo uliochezwa Ijumaa iliyopita nchini DR
Congo ukiwa ni wa Kundi A.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mugalu alisema,
malengo waliyojiwekea katika michuano hiyo ni
kuhakikisha wanashinda michezo yote kwa
kuanzia ugenini hadi nyumbani.
Mugalu alisema kuwa kikubwa wanahitaji pointi
zote 18 katika michezo sita watakayoicheza ya
hatua hiyo, nyumbani na ugenini katika Kundi
A, lenye timu za Al Ahly, El Merrikh na AS Vita.
Aliongeza kuwa, kikubwa wamedhamiria kufuzu
hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa
Afrika baada ya msimu uliopita kushindwa
kufika huko.
“Bado tuna kibarua kigumu kiukweli katika
kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hii,
kikubwa tunachotakiwa ni kujipanga ili kutimiza
malengo yetu.
“Siyo kazi rahisi kwetu, lakini kwa malengo
tuliyoyapanga msimu huu ni kuhakikisha
tunashinda michezo yote ya ugenini kama
tulivyoanza dhidi ya Vita.
“Kama tukipata matokeo mazuri ya ugenini,
ninaamini nyumbani tutakuwa na kazi rahisi
kwa kuutumia vema uwanja wetu wa
nyumbani,” alisema Mugalu.
SOURCE: SPOTI XTRA
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS