Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum SERIKALI imewaalika wawekezaji kutoka nchi za Ghuba na kuwaeleza kwamba ...
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema hayo jana wakati wa mkutano ulioandaliwa na Serikali na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa nchi za Ghuba kujadili uwekezaji nchini.
Katika mkutano huo wa siku mbili uliohudhuriwa pia na wawekezaji kutoka nchi za Ujerumani, Marekani, maofisa wa serikali na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, watapata fursa za kujadili jinsi ya kuondosha vikwazo vya ufanyaji biashara na uwekezaji.
“Napenda kusisitiza kuwa chini ya uongozi imara wa kisiasa wa Rais Jakaya Kikwete ,Tanzania ni sehemu nzuri katika karne hii kuishi na kuwekeza kutokana na siasa safi, upatikanaji wa masoko na mengineyo,” alisema.
Mkuya alisema ripoti hiyo ya mwaka 2012, ilieleza kuwa Tanzania imetoa sura pana ya uwekezaji katika maeneo ya kiuchumi na kupata fedha zenye kuongeza thamani kwa kila mwaka zaidi ya Sh trilioni 1.76.
Katika kuondoa vikwazo, nchi imedhamiria kuondoa kikwazo cha wawekezaji kupata vibali kwa kuhakikisha wanaimarisha vituo vya uwekezaji Tanzania Bara na Visiwani huku wakiwahakikishia wawekezaji mazingira bora ya biashara.
Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh alisema wawekezaji hao kutoka nchi sita za Ghuba, wamedhamiria kuwekeza nchini katika sekta za chakula na ufugaji kwa lengo la kutegemea chakula kutoka nchini kupeleka katika nchi hizo.
COMMENTS