Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij KOCHA wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars M...
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati akitangaza kikosi hicho kocha Nooij alisema kati ya wachezaji hao 10 ambao wanatoka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa wataweka kambi Mwanza na wengine 10 wanaotoka Dar es Salaam wataweka kambi nyingine kabla ya kwenda Mwanza Januari 19 kuungana na wengine kwa ajili ya kambi ya pamoja.
“Mechi hiyo ni muhimu kwetu kwani wachezaji ambao watafanya vizuri tutawapandisha kucheza katika kikosi kikubwa,” alisema Nooij.
Wachezaji walioteuliwa ni Aishi Manula, Benedict Tinoko, Miraji Adam, Andrew Vicent, Michael Gadiel, Emmanuel Semwanda, Joram Mgeveke, Edward Charles na Adam Salamba.
Wengine ni Aboubakary Mohammed, Hassan Dilunga, Hussein Malombe, Shiza Ramadhani, Omari Nyenje, Kelvin Friday, Alfred Masumbakenda, Salim Mbonde, Atupele Green, Rashid Mandawa, Manyika Peter, Salum Telela, Hassan Banda, Mohammed Hussein, Said Ndemla, Said Makapu na Simon Msuva.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Vedastus Lufano, kiingilio kwenye mechi hiyo kitakuwa Sh 20,000 kwa viti maalumu (VIP), viti vya kawaida Sh 10,000 na mzunguko ni Sh 3,000.
Lufano aliwataja baadhi ya wachezaji wa Amavubi wanaotarajia kutua jijini Mwanza Januari 21 kwa ndege ya Rwanda Air, ni Marcel Nzarora, Olivier Kwizera, Sotel Kayomba, Ismail Nshutiyamagala , Emery Basiyenge na Michel Rushengoga.
Wengine ni Fitina Ombolenga, Janvier Mutijima, Haruna Niyonzima, Tean Baptista, Mugiraneza Savio, Nshuti Dominique, Patrick Sibomano, Jean Claude, Zagabe Andrew, Buteara Ernest , Sugira Danny, Ushengimana Betramed Iladukunda na Blenvue Mugenzi.
Lufano aliongeza kuwa taarifa iliyotumwa TFF kutoka Rwanda, Amavubi itaongozana na viongozi wake Stephen Costan, Vincent Mashami, Ibrahim Mugisha, Moussa Hakizimana, Nuhu Assouman, Boume Mugabe, Piere Baziki na Mkuu wa Msafara Bandora Felician.
Awali, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF Boniface Wambura alisema mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo za kuwania kufuzu kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN). Mechi za mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu
COMMENTS