UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kwa sasa unaendelea na maandalizi ya mechi yao dhidi ya Mbuni utakaochezwa Uwanja Azam Complex. Mchezo h...
UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kwa sasa unaendelea na maandalizi ya mechi yao dhidi ya Mbuni utakaochezwa Uwanja Azam Complex.
Mchezo huo ni wa hatua ya 32 bora na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu itakayopoteza safari inawakuta.
Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina imeendelea na mazoezi kwenye viunga vya Azam Complex.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mipango ipo sawa na wanaamini watakutana na ushindani mkubwa ndani ya uwanja.
"Tunawaheshimu wapinzani wetu na tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu hilo lipo wazi ila tunahitaji ushindi ndani ya uwanja.
"Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani na morali ni kubwa ni jambo la kusubiri ili kuona namna gani wataweza kupata matokeo," amesema.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS