Wizara ya Afya Yakutana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kazi cha kuweka mwelekeo wa Ushirikiano
HomeHabari

Wizara ya Afya Yakutana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kazi cha kuweka mwelekeo wa Ushirikiano

Na Mwandishi wetu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao...

Spika Ndugai awaomba radhi Wakristo na Watanzania waliokwazwa na kauli yake
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo September 1
Ahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka mtoto wa mwaka mmoja na miezi saba


Na Mwandishi wetu,

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kazi cha kuweka mwelekeo wa Ushirikiano miongoni mwao na kutafuta ufumbuzi wa changamoto katika kufikia maendeleo yanayokusudiwa.

Kikao hicho cha kihisitoria, kimefanyika Jijini DSM ambapo mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao hicho alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 350 kutoka Serikalini na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Katibu Mkuu Dkt. John Jingu amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo nchini.

Aidha, amesema Serikali kwa nyakati tofauti imeanzisha na kusimamia Sera, Kanuni na Miongozo mbalimbali ili kuwezesha uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji shughuli za Serikali na Sekta ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

 “Ukiniuliza sasa hivi, naweza kukueleza mchango wa NGOs katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo kupitia sekta mbalimbali iwe katika sekta za maji, elimu, afya Ardhi na nyinginenezo nyingi” Alisema Dkt. Jingu.

Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Richard Sambaiga amewataka wadau wa NGOs kutumia kikao kazi hicho kama fursa ya kupata muelekeo wa kuboresha mapungufu na kutatua changamoto zilizopo katika Sekta ya NGOs.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Francis Kiwanga ameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali kukutana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuwa hiyo ndicho chanzo cha mazungumzo kati ya pande hizo mbili na Mkutano wa Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali  ni hatua muhimu na chanzo cha kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Anna Henga amesema Kikao cha aina hiyo kitaepusha malalamiko yaliyokuwa yakijitokeza hapo awali ambapo sasa wadau wamepata fursa ya kuzungumza changamoto zao.

Ameongeza kwa kupongeza Serikali kwa kushiriki mazungumzo na Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali ni lango la kuingia katika meza ya mazungumzo na kuainisha changamoto na kutafuta ufumbuzi wake.

Kikao Kazi cha Siku mbili kati ya Serikali na NGOs , kinalenga kuboresha uhusiano kati ya pande hizo mbili, kutambulisha mchango wa NGOs katika maendeleo ya Nchi, pamoja na Uratibu na Usimamizi wa Mashirika hayo.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wizara ya Afya Yakutana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kazi cha kuweka mwelekeo wa Ushirikiano
Wizara ya Afya Yakutana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kazi cha kuweka mwelekeo wa Ushirikiano
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3jA6zXlrOjZO90DI4WGkcnQDcUVHXHRakxQrh0sGe7iniylXrihl3NDUs1yBhUOF3wGXNR2Tcr60pAnO2v3kBAeEmakKw9BXACQHoAzkIYgFqJ6D_fYgFMyKkRO9BOh2waHYe79kUUqH2/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3jA6zXlrOjZO90DI4WGkcnQDcUVHXHRakxQrh0sGe7iniylXrihl3NDUs1yBhUOF3wGXNR2Tcr60pAnO2v3kBAeEmakKw9BXACQHoAzkIYgFqJ6D_fYgFMyKkRO9BOh2waHYe79kUUqH2/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/01/wizara-ya-afya-yakutana-na-mashirika.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/01/wizara-ya-afya-yakutana-na-mashirika.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy