BAADA ya wiki iliyopita msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma kuripotiwa kwenye moja ya magazeti pendwa kuwa hana uhusiano na mtu ye...
BAADA ya
wiki iliyopita msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma kuripotiwa kwenye
moja ya magazeti pendwa kuwa hana uhusiano na mtu yeyote ndani ya Bongo
Muvi na yupo mbioni kumuanika mrithi wa Sajuki mengi yameendelea
kuibuka.
Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma akiwa kwenye pozi la kimahaba na Bondi Bin Salim.
Akizungumza
na Uwazi, mpenzi wa Wastara anayetambulika kwa jina la Bondi Bin Salim
alidai kuwa yupo kwenye mchakato wa mwisho wa kutoa mahari kwa ndugu wa
msanii huyo kiasi cha shilingi milioni 5 pamoja na pete za dhahabu ili
aweze kuwa na Wastara.
Alisema
kuwa maamuzi ya kutoa posa yamekuja baada ya kuona kila mmoja anaweza
kuishi na mwingine kwani wameshasomana kwa muda mrefu.
“Najua
si jambo la watu kuhoji sana kwa sababu ndoa ipo na kila mtu atafanya
hivyo, nina hela ya mahari tayari na siku ikipangwa ya kutoa tutafanya
hivyo lakini ninachowaza sasa ni kuona nafanya vipi ili harusi yangu iwe
ya kipekee na zoezi hili tutalifanya mwakani,” alisema.
COMMENTS