Urais 2015: Mwanamke wa kwanza CCM ajitokeza kutangaza nia
Mwanamke wa Kwanza ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) Amina Salum Ali atangaza kugombea urais.
HomeHabarikisiasa

Urais 2015: Mwanamke wa kwanza CCM ajitokeza kutangaza nia

Mwanamke wa Kwanza ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) Amina Salum Ali atangaza kugombea urais.   ********** Mwanamke wa Kwanza ...

Lowassa Na Wenzake Sasa Wako Huru....Adhabu Yao Ilikwisha Jana......Taarifa Kamili iko Hapa
Mrema Avuliwa Uanachama TLP
Uenyekiti wa Mrema wapingwa mahakamani
  **********

Mwanamke wa Kwanza ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) Amina Salum Ali, amevunja ukimya na kuamua kuweka wazi nia yake ya  kutaka kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba.
 

Akizungumzia uamuzi huo, mwanasiasa huyo ambaye pia ni Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) katika Umoja wa Mataifa (UN), amesema wanawake wamekuwa wanyonge kugombea nafasi za juu za uongozi kwa kukosa fedha, lakini sasa ni wakati mwafaka kwao kujiamini katika jamii kwani uongozi siyo fedha bali ni uzalendo, kujikubali na kujiamini.
 

“Nimeona nina uzalendo, ninajiamini na ninaweza kuifikisha nchi yangu katika uchumi wa kwanza kwa kutumia rasilimali zetu zikiwamo gesi, mafuta, kilimo na utalii. Ninajiamini kwamba wakati wangu umefika kuwaongoza Watanzania.” amesema Amina
 

Amina  aliwahi kushika nafasi za juu za uongozi Zanzibar na Tanzania Bara, ukiwamo uwaziri wa fedha Zanzibar.
 

Ameongeza kuwa wanawake wengi wanaogopa kujitokeza wakihofia kugombea nafasi za juu za uongozi kwamba kunahitaji fedha hivyo wanaishia kuwa wanyonge."Siyo kweli, wajitokeze kwa wingi ili kitimiza ndoto za kuwajibika kwa taifa letu,” alisema.
 

Amina anaungana makada wengine  wanaotajwa kuwania Urais  mwaka huu ambao   ni mawaziri wakuu wastaafu, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja ,  Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi , Teknolojia, January Makamba pamoja na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangalah.
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Urais 2015: Mwanamke wa kwanza CCM ajitokeza kutangaza nia
Urais 2015: Mwanamke wa kwanza CCM ajitokeza kutangaza nia
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8IYFTcV57Dkp6LXoFHutEl_W61OJ8FCokwLhZQZXy53z3IdKERzDqI8EXprBe-jfHgVp8QDgKU0kVF2RM40lWBYGRnQppSy2W73m3_We_TaVCTg4TcNmiDFTeagBBLdiRjQyULfD-mRGA/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8IYFTcV57Dkp6LXoFHutEl_W61OJ8FCokwLhZQZXy53z3IdKERzDqI8EXprBe-jfHgVp8QDgKU0kVF2RM40lWBYGRnQppSy2W73m3_We_TaVCTg4TcNmiDFTeagBBLdiRjQyULfD-mRGA/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/05/urais-2015-mwanamke-wa-kwanza-ccm.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/05/urais-2015-mwanamke-wa-kwanza-ccm.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy