Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha TLP , Augustine Mrema Mwasisi wa chama cha TLP, Stanley Nda...
Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha TLP , Augustine Mrema
Mwasisi
wa chama cha TLP, Stanley Ndamugoba amemburuza mahakamani Mwenyekiti wa
Taifa wa chama hicho, Augustine Mrema akidai si kiongozi halali.
Kesi
hiyo ya madai namba 33/2015 ilifunguliwa na Ndamugoba Ijumaa iliyopita
katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam ikiambatanishwa na
hati ya usikilizwaji wa haraka.
Katika
kesi hiyo ambayo Baraza la Wadhamini limeunganishwa kama mdaiwa wa
pili, Ndamugoba ameiomba mahakama itamke uongozi wa Mrema ulifikia
kikomo mwaka mmoja uliopita. Mdai anaiomba mahakama kuu itamke kuwa kwa
vile muda wake wa uongozi ulimalizika mwaka mmoja uliopita, Mrema hana
mamlaka ya kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi.
Ndamugoba
mwenyewe alilithibitishia gazeti hili jana kufungua kesi hiyo akisema
leo atakwenda Mahakama Kuu ili kuchukua samansi za kumuita Mrema
shaurini pamoja na Baraza la Wadhamini.
“Ni kweli nimefungua kesi na nafikiri kesho (leo) samansi zitatoka,” alisema.
Hata
hivyo Mrema alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusu kuwapo kwa kesi
hiyo, alisema yeye hakujiongezea muda kwa nguvu bali katiba ya TLP ndiyo
ilimwongezea muda huo.
“Mimi
sikujiongezea muda kwa nguvu wala sikuongezewa na mtu yeyote. Sisi
tunafuata katiba ya TLP. Tatizo hapa ninaloliona ni vita ya ubunge Jimbo
la Vunjo,” alisema Mrema.
Mrema
alifafanua kuwa kamati kuu iliyopita, ilifanya uamuzi na kumpitisha
yeye kuwa mgombea ubunge Jimbo la Vunjo na mgombea pekee wa nafasi ya
uenyekiti wa TLP Taifa.
Bila
kutaja kifungu cha katiba, Mrema alisema halmashauri kuu ya TLP imetoa
madaraka kwa kamati kuu kufanya kazi kwa niaba yake na mkutano mkuu wa
TLP.
“Katiba
iko wazi kwamba endapo kuna mazingira yatajitokeza, kamati kuu imepewa
mamlaka ya kufanya kazi za halmashauri kuu na mkutano mkuu na uamuzi huu
ulifikiwa 2007,” alisema. “Tulitumia kipengele hicho kusogeza mbele
mkutano mkuu wa uchaguzi kwa mwaka mmoja na tumeshatangaza mkutano mkuu
wa uchaguzi utafanyika Aprili 23, mwaka huu,” alisisitiza.
Mrema
alisema maelezo hayo ndiyo ambayo waliyatoa pia kwa Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jaji Francis Mutungi baada ya baadhi ya wanachama kulalamika
na huo ndiyo msimamo wa kikatiba
COMMENTS