Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Simon Msuva amempasha Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Z...
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Simon Msuva amempasha Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Zacharia Hanspope kuwa hataihama Yanga na kwenda Simba labda iwe nje ya nchi.
Hivi Karibuni mwenyekiti huyo alitamba kuwa, bado wanaendelea na mchakato wao wa kumfukuzia Msuva ili aweze kusaini kuitumikia klabu hiyo msimu ujao baada ya jaribio lao la awali kugonga mwamba.
Msuva alisema hataihama Yanga na kujiunga na timu yoyote nchini.
“Labda nipate timu nje ya nchi, vinginevyo nitaendelea kuitumikia Yanga. Sina mpango wa kwenda Simba wala timu nyingine ya nyumbani,” alisema
COMMENTS