Baada ya malalamiko ya wabunge wa upinzani juu ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai, anat...
Baada ya malalamiko ya wabunge wa upinzani juu ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai, anatarajia kuzipangua kamati hizo.
Taarifa
za uhakika toka Bungeni mjini Dodoma zinasema, licha ya kuwapo kwa
baadhi ya wajumbe walioomba kuhamishwa kwenye kamati walizopangiwa
awali, kumekuwapo na mazungumzo kati ya Kambi ya Upinzani Bungeni na
kiti ofisi ya Spika juu ya suala hilo.
Inaelezwa
kati ya wajumbe watakaohamishwa kutoka kwenye kamati zao za awali ni
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe aliyekuwa kwenye
Kamati ya Maendeleo ya Jamii na sasa atapelekwa Hesabu za Serikali
(PAC).
Naye
Mbatia aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Miundombinu, sasa atapelekwa
kwenye Kamati ya Bajeti aliyokuwa akitumikia kwenye Bunge la 10.
Spika wa Bunge, alipotafutwa ili kuzungumzia suala hilo kupatikana.
Juzi
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bunge, Tundu Lissu, alisema wanafikiria
kumpeleka Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kwenye
kamati ya PAC ili awe mwenyekiti wao.
“Wasipokubali
(kubadilisha wajumbe) hatutakubali ungozi tutaacha, mimi mwenyewe
sheria ndogo siendi, huko ni kupoteza muda kwa sababu hakuna kamati ya
ovyo vile, nitaenda sheria na katiba na kushiriki mijadala, kura tu
ndiyo sintopiga, hoja yoyote ya kisheria ikiibuka bungeni nitaibuka na
watashangaa,” alisema Lissu.
COMMENTS