Baada ya chama hicho kuzinduliwa rasmi, nguvu yake imeelekezwa katika kujijenga na kujiimarisha zaidi,” Mwenyekiti wa ACT-Tanzan...
Baada
ya chama hicho kuzinduliwa rasmi, nguvu yake imeelekezwa katika
kujijenga na kujiimarisha zaidi,” Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Anna
Mghwira
Chama
cha ACT- Tanzania, kimesema hakina muda wa kufanya siasa za chuki na
malumbamo dhidi ya vyama vingine vya siasa, badala yake kinajipanga
vizuri na kuandaa mazingira ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti
wa chama hicho Anna Mghwira, aliliambia gazeti hili mwishoni mwa juma
kuwa, baada ya chama hicho kuzinduliwa rasmi Machi 29 mwaka huu, nguvu
yake sasa imeelekezwa katika kujijenga na kujiimarisha.
Alisema
katika kujiimarisha, chama hicho kinatafuta wanachama, kwa kuwa
kinatambua kuwa ni mtaji wa kujihakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu,
pamoja na kuandaa wagombea kwa kuangalia uwezo wao kadri
watakavyojitokeza.
“Mimi
mwenyewe ni miongoni mwa wagombea ubunge, nitagombea Jimbo la Singida
mjini na naamini kwamba nitaweza kupata nafasi hiyo kwa sababu
ninafahamika kule ni nyumbani nilikozaliwa . Nimesoma huko, nimekulia
huko na najua changamoto zinazotukabili wakazi wa kwetu na jinsi
nitakavyoshiriki kukabiliana nazo nikiwa mbunge,”
Mghwira
alieleza kuwa chama hicho kinajiimarisha, huku kikitambua kuwa kina
wajibu wa kuendeleza ushirikiano na vyama vingine vya siasa, badala ya
kujitenga na kuendesha shughuli zake kama kisiwa.
Mwenyekiti
huyo, alitolea mfano siku ya uzunduzi wa chama hicho akisema kuwa
kulikuwa na watu wengi kutoka vyama mbalimbali ambao walitaka kurudisha
kadi za vyama hivyo hadharani na kuchukua kadi za ACT, lakini
walisitisha shughuli hiyo kuepuka uhasama.
“Kuwa
vyama tofauti haina maana kwamba tuwe maadui, kulikuwa na wanachama
wapya siku ya uzinduzi (wa ACT) walitaka kuonyesha hadharani
wanavyorudisha kadi za vyama vyao vya awali hatukuwapa nafasi hiyo, kwa
sababu hatuoni kuwa hilo ni jambo la kuvutia kwetu,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mghwira siku hiyo walipokea wanachma wapya 2,000 na bado
wanaendelea kupokea wanachama wengine kutoka vyama mbalimbali vya siasa
lakini kwa siri.
Ingawa
Mghwira hakutaja watu, asilimia kubwa ya viongozi wa kitaifa wa chama
hicho, akiwamo Zitto Kabwe ambaye sasa ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho
na Katibu Mkuu Samson Mwigamba na Profesa Kitila Mkumbo, wamejiunga na
chama hicho baada ya kufukuzwa na vyama vyao.
“Pia
katika kuonyesha nia yetu ya kuhitaji ushirikiano mwema wa kisiasa
tuliwaalika viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani, ikiwemo Chadema
na CUF,” alisema. Alisisitiza kuwa Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) ni miongoni mwa wasomi na
viongozi wa vyama vingine vya siasa walioalikwa kutoa mada katika
uzinduzi wa chama hicho, lakini alipata udhuru hivyo hakufika.
“Hata hivyo tulifarijika kuona shughuli yetu ya uzinduzi wa chama ikifanyika vizuri na kwa amani,” alisema.
COMMENTS