Zaidi ya vijana 500 wakamatwa Tanzania
Kamanda wa Polisi Suleiman Kova
HomeHabariKitaifa

Zaidi ya vijana 500 wakamatwa Tanzania

Kamanda wa Polisi Suleiman Kova Vijana zaidi ya mia tano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa t...


Vijana zaidi ya mia tano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa tuhuma za kujihusisha na Vitendo vya uhalifu vilivyozua taharuki na hofu kubwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Vijana hao wanatuhumiwa kusababisha hofu kubwa jijini Dar es Salaam kwa kile kilichoelezwa kitendo cha kulipiza kisasi kufuatia kifo cha mwenzao aliyefariki kwa kupigwa mawe na wananchi waliojichukulia sheria mkononi.
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salam Suleiman Kova amethibitisha kukamatwa kwa Vijana hao kwa tuhuma za uhalifu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Polisi wakiwa katika doria

Vijana hao zaidi ya mia tano wakiwa washiriki wakuu katika Kundi la vijana waporaji lijulikanalo kama Panya Road wanashikiliwa na Jeshi la polisi kufuatia msako mkali unaoendelea jijini kote Dar es Salaam baada ya tukio la mwishoni mwa wiki ambapo jiji la Dar es Salaam lilikumbwa na taharuki kubwa baada ya vijana hao kuanza kufanya vitendo vya uporaji mitaani.
Kova amesema katika msako huo unaoendelea mbali na kuwakamata vijana hao katika msako huo pia wamekamatwa wakiwa na Puli,kete na misokoto ya Bangi pamoja na Mirungi na Lita 150 za pombe haramu ya Gongo.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo mbali mbali jijini Dar Es Salaam katika sehemu mbali mbali kama kwenye vituo vya mabasi ,kwenye majumba mabovu na pia kwenye makazi yao kutokana na msako huo kufanyika nyumba kwa nyumba.

Hii ni mara ya kwanza kwa kundi kubwa la watuhumiwa kukamatwa kwa wakati mmoja na kushikiliwa huku wakisubiri kufikishwa mahakamani
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Zaidi ya vijana 500 wakamatwa Tanzania
Zaidi ya vijana 500 wakamatwa Tanzania
http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/304/amz/worldservice/live/assets/images/2014/07/22/140722135006_tanzania_polisi_304x171_bbc_nocredit.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/zaidi-ya-vijana-500-wakamatwa-tanzania.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/zaidi-ya-vijana-500-wakamatwa-tanzania.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy