Ripoti: Tanzania kinara wa utumwa
A.Mashariki
HomeRipoti

Ripoti: Tanzania kinara wa utumwa A.Mashariki

Ri poti mpya ya kimataifa kuhusu hali ya utumwa duniani imeitajaTanzania kuongoza Afrika Mashariki. Dar es Salaam. Ripoti mpya ya kimata...

Ripoti mpya ya kimataifa kuhusu hali
ya utumwa duniani imeitajaTanzania
kuongoza Afrika Mashariki.

Dar es Salaam. Ripoti mpya ya
kimataifa kuhusu hali ya utumwa

duniani imeitajaTanzania kuongoza
Afrika Mashariki kwa kuwa na zaidi
ya watu 350,000 wanaotumikishwa
maeneo mbalimbali nchini.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia
na Watoto, Sophia Simba, jana alikiri
kuwapo kwa tatizo hilo akisema: “Ni
kweli kuwa wafanyakazi wa ndani
wanatumikishwa hapa nchini
ikilinganishwa na nchi nyingine.”
Ripoti hiyo ijulikanayo kama ‘The
Global Slavery Index 2014’,
iliyotolewa nchini Australia Novemba
mwaka huu, inaonyesha kuwa
Tanzania inashika nafasi ya 14
barani Afrika na kuwa ya 33
duniani.
Imeitaja Uganda kuwa ndiyo
inayoshika nafasi ya pili kwa kuwa
na watumwa 135,000, ikifuatiwa na
Rwanda (83,600), Burundi (72,300)
huku Kenya ikiwa na watumwa
64,900.
Utafiti huo uliofanyika katika nchi
167 duniani, unatafsiri utumwa kuwa
ni hali ya mtu kumhifadhi mtu
mwingine na kumnyima uhuru binafsi
kwa nia ya kumnyonya kwa njia ya
madaraka, faida au kumsafirisha.
“Mataifa mbalimbali yanatumia
maneno tofauti kuuelezea utumwa
mambo leo, ikiwa ni pamoja na
kusafirisha binadamu, utumikishwaji,
ndoa za lazima, kuuzwa kwa watoto.
Maovu yote yanazungumzia jambo
moja,” inasema ripoti hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa hivi sasa
kuna watumwa milioni 35.8 duniani
kote, kati yao milioni 14 wapo India,
milioni 3 wapo China na milioni 2
wanapatikana Pakistan.
Akizungumzia ripoti hiyo Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Sophia Simba alisema hali
imefika ilipo sasa kutokana na
kukosekana kwa sheria kali na
vyama vyenye nguvu vya kutetea
haki za wafanyakazi hao.
Waziri Simba alisema kwa sasa ni
jambo la kawaida kumsikia mtu
akijisifu kuwa amekaa na
mfanyakazi kwa miaka mitatu bila
kwenda likizo.
“Mtu anasema ‘nimekaa naye miaka
mitatu msichana huyu ni mzuri’ kwa
hiyo nini? Anakaa kwako kwa sababu
umeshindwa hela ya kumlipa
akapange kama wafanyakazi
wengine,” alisema.

Aliongeza: “Msichana anakuwa wa
kwanza kuamka asubuhi na wa
mwisho kulala usiku, akupikie
mchana, usiku na akufungulie
mlango unaporudi. Ndiyo maana
wasichana wanawadhuru watoto
wanaokaa nao.”
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia
Kabaka na naibu wake, Dk
Makongoro Mahanga hawakuweza
kupatikana kuzungumzia ripoti hiyo
baada ya simu zao kuita bila
kupokelewa.
Kuhusu Afrika, ripoti inaonyesha
kuwa Nigeria ndiyo inayoongoza kwa
kuwa na watumwa 834,200,
ikifuatiwa na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) (7,620,
900), Sudan (429, 000), Misri (393,
800) na Tanzania (350,000).
Nchi yenye watumwa wachache zaidi
dunia ni Iceland ambayo inachini ya
watu 100 wanaotumikishwa. Mauritus
yenye watumwa 3,300 ndiyo
iliyotajwa kuwa ya mwisho Afrika
kwa kuwa na watu wachache.
Ripoti hiyo, pia imetaja nchi
zinazoongoza kwa kuwa kuweka
mikakati imara ya kupunguza idadi
ya watu wanaotumikishwa. Nchi hizo
zimetambuliwa kwa kupewa maksi
kulingana na alama zilizopata.
Netherland imetajwa kuwa na sera
nzuri zaidi duniani baada ya kupata
alama AA.
Nchi nyingine zilizofuatia na alama
zao kwenye mabano ni Sweden (A),
Marekani (BBB), Australia (BBB) na
Switzeland (BBB).
Kwa upande wa Afrika, Nigeria ndiyo
imetajwa kuwa na sera nzuri baada
ya kupata alama B, ikifuatiwa na
Zambia (CCC), Senegal (CCC),
Uganda (CCC) na Ghana (CCC).
Vilevile Uganda imetajwa kuwa na
mikakati bora ya kupunguza idadi ya
watumwa Afrika Mashariki baada ya
kupata alama CCC ikifuatiwa na
Kenya (CC), Rwanda (CC), Burundi
(CC) huku Tanzania ikishika ‘mkia’
kwa kuibuka na alama C. Kwa mujibu
wa ripoti hiyo, alama C inamaanisha
kuwa jitihada za Serikali kuondoa
tatizo ni ndogo sana, huku kukiwa na
idadi ndogo ya waathirika waliopata
msaada.
Baadhi ya sera na vitendo vya
Serikali vinarahisisha kuongezeka kwa watumwa.

Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Ripoti: Tanzania kinara wa utumwa A.Mashariki
Ripoti: Tanzania kinara wa utumwa A.Mashariki
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwo1prLcMKjUf8HQYLkkqP8PWoeQSwgbBDxQtkql08acu2gQlQmz7PktFkcw_fDTaHfVP6V9BAi2fORc1xXCFouhyURPE9ZaID0SkmyM5WsnRA24l_uB_A3B58p2iR0MKVtnyO-BGRnYde/s640/simba.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwo1prLcMKjUf8HQYLkkqP8PWoeQSwgbBDxQtkql08acu2gQlQmz7PktFkcw_fDTaHfVP6V9BAi2fORc1xXCFouhyURPE9ZaID0SkmyM5WsnRA24l_uB_A3B58p2iR0MKVtnyO-BGRnYde/s72-c/simba.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2014/12/ripoti-tanzania-kinara-wa-utumwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2014/12/ripoti-tanzania-kinara-wa-utumwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy