Saluni ya Ngono Yafumuliwa jijini Dar......Wahudumu wake ni makahaba, mteja hulipa Elfu 60>>>>Angalia LIVE hapa
HomeMatukio

Saluni ya Ngono Yafumuliwa jijini Dar......Wahudumu wake ni makahaba, mteja hulipa Elfu 60>>>>Angalia LIVE hapa

HALI ni mbaya! Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya...

Lulu amtaka Marlaw kurudi kwenye game
Ajuza miaka 90: anasoma darasa la nne. Je Elimu Kweli Haina Mwisho?
Ndugu wa marehemu wameukosa mwili wa mtu wao, kaburi halikuachwa wazi! soma na angalia video hapa>>> Video
HALI ni mbaya! Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.

Mhudumu wa saluni ya kuchua akificha sura yake mara baada ya kunaswa na OFM akijihusisha na biashara haramu ya ngono.


 UCHUNGUZI
Makachero wa kitengo maalum cha Global Publishers cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) walifanya uchunguzi na kugundua kuwa zipo saluni nyingi jijini Dar zinazojishughulisha na biashara ya massage (kuchua) lakini ndani yake wahudumu wanajiuza hadi miili ambapo wateja wakubwa ni waume za watu na vigogo serikalini.
Mhudumu akijificha chini ya kitanda kukwepa camera za OFM.

TUKIO BICHI
Hivi karibuni OFM walipokea simu kutoka kwa mmoja wa wanawake aliyedai kuchoshwa na shughuli zinazofanyika katika saluni moja ya kuchua (massage, jina linahifadhiwa kwa sasa) iliyopo katika eneo la Kinondoni-Morocco, Dar.
Mhudumu huyo mwenye asili ya kisomali akitinga viwalo mara baada ya kunaswa.
“Jamani nipo hapa nje, nimemfuatilia mume wangu, maana kila siku nasikia huwa anaonekana hapa, hii ni saluni ya kuchua, lakini humo ndani wale wahudumu ni makahaba, wanajiuza tena wanafanyia humohumo ndani, naombeni mje, nataka kufumania,” chanzo chetu kiliongea kwa hasira na uchungu..
..Huyu hapa ndio mhudumu mwenyewe.

OFM MZIGONI
Kama ilivyo kawaida ya OFM kutodharau wito wowote unaohusiana na uvunjaji wa maadili, uonevu na uhalifu, kikosi kilipangwa harakaharaka na kwa kutumia pikipiki ziendazo kasi, zikafika eneo la tukio katika muda muafaka, kwani difenda la polisi, nayo ilionekana ikiingia eneo hilo kuitikia wito wa raia wema.
Baadhi ya vifaa vya kufanyia masaji vikiwa mezani.
KABAAAH!
Ndani ya saluni hiyo, OFM ilishuhudia mhudumu wa mapokezi ambaye baada ya kuonyeshwa vitambulisho vya askari wa Jeshi la Polisi, alinywea na kuwaruhusu kupekua chumba kimoja baada ya kingine, ili kujionea kama kweli nyumba hiyo ilikuwa ikijihusisha na masuala ya saluni ya uchuaji pekee na siyo vinginevyo.
Moja ya vitanda vinavyotumiwa kwa ajili ya biashara ya ngono kwa wateja wanaofika katika saluni hiyo.

Katika chumba cha kwanza, askari hao walimkuta mwanaume mmoja akiwa uchi wa nyama, lakini mwanamke aliyekuwa naye akiwa amevaa nguo zake, kitu kilichoashiria kuwa tayari ‘mchezo ulishafanyika’.
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kupitia vyumba vingine vinne na kuvikuta tupu, kilichofuata, OFM walishuhudia mwanamke mwenye asili ya Kisomali akiwa uchi na mwanaume wake, dalili zote zikionyesha kuwa walikuwa wakijiandaa kufanya uzinzi.
Mhudumu mwingine aliyenaswa katika saluni hiyo.

WAZINZI WAJITETEA
Baada ya kuwakuta katika hali hiyo, kiongozi wa askari hao, (jina kapuni) aliwauliza kama hiyo ndiyo biashara ya masaji waliyopata kibali cha kuifanya, lakini wakabakia kujiumauma pasipo kutoa jibu la kueleweka.
Binti huyo wa Kisomali, ghafla aliibuka na kuanza kuomba msamaha kwa kitendo hicho, akidai maisha magumu wanayoishi, ndiyo yanayosababisha waifanye biashara hiyo. 

Wahudumu walionaswa wakipakizwa kwenye karandinga kuchuliwa hatua za kisheria.

KUMBE ANA MTOTO
Lakini la kushangaza zaidi, ni pale mwanamke huyo alipodai kuwa nyumbani alikotoka, ambako ameolewa, pia alimuacha mwanaye mwenye umri wa miezi minne.

“Nisameheni jamani, mimi ni mke wa mtu na isitoshe nimeacha kichanga nyumbani, ni shida tu ndiyo imenileta hapa,” alisikika akiomba mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Salma.
Mwanaume aliyekutwa naye, alipoulizwa biashara hiyo inafanyika kwa bei gani, alisema makubaliano yake na mwanamke huyo, ni kutoa kiasi cha shilingi elfu sitini kwa tendo moja!
OFM iliondoka eneo hilo baada ya askari hao kuwapakiza katika karandinga wanawake wanne na wanaume wawili tayari kwa safari ya kituoni kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.


Angalia LIVE Hapa 





Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Saluni ya Ngono Yafumuliwa jijini Dar......Wahudumu wake ni makahaba, mteja hulipa Elfu 60>>>>Angalia LIVE hapa
Saluni ya Ngono Yafumuliwa jijini Dar......Wahudumu wake ni makahaba, mteja hulipa Elfu 60>>>>Angalia LIVE hapa
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDXxe4qSQ7MKLncABlORGZ3ObuVKuItEVnyjN9Y7fDRECSKuUceTQNxm0rPubRYe9mN5kfmh3airUsAl1r2A_Rj9pcfA5NtcXElqSvkT76vJnYZs5QbNgZo_25qsr26w1Ih4FzX5ZGofWL/s640/frontjumamosi.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDXxe4qSQ7MKLncABlORGZ3ObuVKuItEVnyjN9Y7fDRECSKuUceTQNxm0rPubRYe9mN5kfmh3airUsAl1r2A_Rj9pcfA5NtcXElqSvkT76vJnYZs5QbNgZo_25qsr26w1Ih4FzX5ZGofWL/s72-c/frontjumamosi.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/saluni-ya-ngono-yafumuliwa-jijini.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/saluni-ya-ngono-yafumuliwa-jijini.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy