MSD yatakiwa kusimamia uendeshaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini
HomeHabariTop Stories

MSD yatakiwa kusimamia uendeshaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Bohari ya Dawa nchini (MSD) kusimamia viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa za afya ikiwemo d...

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua Skuli ya Sekondari ya Makoba Kaskazini Unguja
TAAWANU yazindua rasmi zoezi la ugawaji bure wa vitanda elfu 60 kwenye hospitali nchini Tanzania
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 6, 2024

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Bohari ya Dawa nchini (MSD) kusimamia viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa za afya ikiwemo dawa, maji dawa (dripu) ili kuviwezesha viwanda hivyo kuendelea kukua na kuimarisha uchumi wa nchi.

Waziri Mhagama amesema hayo Februali 18, 2025 baada ya kutembelea viwanda vinavyozalisha bidhaa za afya ikiwemo kiwanda cha Pharmaceutical, Medical Devices, Medical Equipment Assembly, Raw materials (API), Common Utilities pamoja na Logistic Centre (Warehousing) vilivyopo Zegereni, kibaha Mkoani Pwani.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja ma maeleekezo yake katika Sekta vilevile kwenye sekta binafsi itumike kuhakikisha inachangia katika ujenzi wa uchumi, ustawi wa wananchi na maendeleo endelevu yaTaifa letu” amesema Waziri Mhagama na kuongeza

“Kwa hiyo hata sisi leo, tumekuja kuona wenzetu wa Sekta binafsi ni namna gani wanaweza kutumika kwenye maendeleo na hasa upande wa sekta ya afya, Serikali yenu inatambua kuna uwekezaji mkubwa ndani ya mkoa wa Pwani ambao unazaidi ya viwanda 100 vilivyojengwa ndani ya muda mfupi,” amesema Waziri Mhagama

Waziri Mhagama amefafanua kuwa, Sekta ya Afya inauhitaji mkubwa wa uwekezaji wa viwanda nchini kwakuwa kwenye bara la Afrika zaidi ya asilimia 70-80 bidhaa za afya zinatoka nje ya nchi pamoja na kuwa na ucheleweshaji wa kufika nchini hivyo Sekata binafsi vema ikaliona hilo na kutumia kama fursa.

Amesema, faida nyingine za uzalishaji wa bidhaa hizo nchini ni pamoja na kupunguza utegemezi, na kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa hizo kwa kuzingatia mahitaji na matumizi ya nchi, kuchagua ni bidhaa gani ambazo zinahitajika zaidi pamoja na kuhifadhi fedha za kigeni ili zitumike kwenye uwekezaji wa maeneo mengine.

Aidha, Waziri Mhagama amesema Serikali imeanza kujipanga kuanza mkakati wa kuuza bidhaa za afya nje ya nchi kwa kuwa tayari Serikali ya Tanzania imepata masoko ya kuuza bidhaa hizo nje ya nchi.

“MSD imepata mamlaka ya kusambaza bidhaa za afya kwenye soko la SADIC, hivyo ni lazima MSD ikae na wazalishaji wa ndani, badala ya bidhaa hizo kuziagiza nje ya nchi ziwe zinatoka ndani ya nchi,” amesema Waziri Mhagma

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) Bw. Mavere Tukai amesema wataendelea kuboresha ushirikiano kati ya Bohari na wazalishaji wa bidhaa za afya nchini ili kufikia lengo ambalo Serikali inalitaka la kuhakikisha bidhaa zote zinanunuliwa nchini na kuweza kuuza bodhaa hizo nje ya nchi.

“Nikushukuru sana Mhe. Waziri wa Afya Jenista Mhagama kwakuwa tangu umekuja kwakweli kutubana umetubana sana na sasa tunaona mafanikio na naamini hatujakuongusha na naahidi kwamba kati ya leo hadi Aprili moja, tutakua tumemaliza bidhaa zile za Katwaza ikiwa ni pamoja na malipo,” amesema Bw. Tukai

 

The post MSD yatakiwa kusimamia uendeshaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/VoqjWYg
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: MSD yatakiwa kusimamia uendeshaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini
MSD yatakiwa kusimamia uendeshaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/02/0c02236c-11bd-4ceb-a9ef-656d61d5b4d2-950x633.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/msd-yatakiwa-kusimamia-uendeshaji-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/msd-yatakiwa-kusimamia-uendeshaji-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy