HomeHabariTop Stories

Mr Beast ataka kuinunua TikTok iwapo itapigwa marufuku Marekani

Mtayarishaji maarufu wa maudhui ya YouTube Jimmy Donaldson maarufu kama MrBeast ameibua gumzo baada ya kutangaza nia ya kuinunua TikTok iwap...

Picha: Rais Samia ahudhuria uzinduzi wa Utalii wa Kasa Kizimkazi, Visiwani Zanzibar
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 24, 2024
Wazazi pelekeni vijana wenu shule – Majaliwa

Mtayarishaji maarufu wa maudhui ya YouTube Jimmy Donaldson maarufu kama MrBeast ameibua gumzo baada ya kutangaza nia ya kuinunua TikTok iwapo itapigwa marufuku Nchini Marekani na hii ni kutokana na TikTok kukabiliwa na tishio la kufungwa kwa huduma zake kwa Watumiaji wa Marekani ifikapo Januari 19, 2025 endapo Mahakama haitasitisha marufuku hiyo.

 

Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa X, MrBeast aliandika “Sawa, nitanunua TikTok ili isipigwe marufuku.” Kisha baadaye aliongeza kuwa Mabilionea kadhaa wamejitokeza na kumshawishi kushirikiana nao katika kufanikisha mpango huo ingawa bado haijabainika wazi kama alikuwa akimaanisha kwa dhati au ni sehemu ya utani wake wa kawaida.

 

Aidha kupitia Sheria iliyosainiwa na Rais Joe Biden mwaka 2024 inaitaka kampuni ya ByteDance kutoka China ambayo ndio kampuni mama ya TikTok kuuza shughuli zake za Marekani ili kuepusha marufuku hiyo ambapo Serikali ya Marekani inadai kuwa TikTok inahatarisha usalama wa Taifa kwa kuruhusu China kukusanya data za Watumiaji wake madai ambayo kampuni ya ByteDance imekanusha mara kadhaa.

 

Endapo marufuku hiyo itatekelezwa itafanya Watumiaji wa TikTok Nchini Marekani kutoweza kupakua Programu hiyo tena huku waliopo hivi sasa wakiendelea kuitumia kwa muda mfupi kabla ya kufungwa rasmi.

 

TikTok bado haijatoa tamko rasmi kuhusu hali hii lakini mpango wa MrBeast umeleta matumaini kwa baadhi ya Watumiaji wa Marekani huku wengine wakisubiri kuona kama nia yake itageuka kuwa hatua halisi ya kibiashara.

 

The post Mr Beast ataka kuinunua TikTok iwapo itapigwa marufuku Marekani first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/rbiqI28
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mr Beast ataka kuinunua TikTok iwapo itapigwa marufuku Marekani
Mr Beast ataka kuinunua TikTok iwapo itapigwa marufuku Marekani
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/mr-beast-ataka-kuinunua-tiktok-iwapo.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/mr-beast-ataka-kuinunua-tiktok-iwapo.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy