Gavu ataka kasi zaidi kuongeza wanachama jumuiya za chama
HomeHabariTop Stories

Gavu ataka kasi zaidi kuongeza wanachama jumuiya za chama

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) Oganaizesheni na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Issa Gavu ameitaka Jumuiya ya Wanawake Tan...

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) Oganaizesheni na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Issa Gavu ameitaka Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT)kuongeza kasi ya kuongeza wanachama wake na kufikia Milioni tisa kutoka wanachama Milioni 6.1 walioko sasa.

Mbali na kuongeza wanachama kwa Jumuiya hiyo ametumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa wale wote ambao wanataka kushirikiana na Chama na Jumuiya zake basi wafuate maelekezo na muongozo wa Chama na kusisitiza katika Chama hicho hakuna mkubwa na maamuzi yote yanatolewa kupitia vikao vya Chama hicho.

Akizungumza Desemba 15,2024 katika Mkutano wa Baraza la Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) Gavu aliyekuwa amemwakilisha Katibu Mkuu Dk.Emmanuel Nchimbi ,amesema amefurahishwa na taarifa ya mafanikio yaliyoelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Marry Chatanda yakiwemo ya kuongeza wanachama wapya.

“Naamini hii ni chachu katika safari ya kutafuta ushindi wa Chama chetu kwa mwaka 2025 ,nawapongeza kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuingia kwenu madarakani .Katika taarifa yenu mmeonesha  idadi kubwa ya wanachama wapya walioingizwa katika Jumuiya hiyo kutoka wanachama Milioni 4.1 mpaka wanachama Milioni 6.1.

“Maana yake kuna wanachama takribani milioni  mbili na hili mmelifanya katika  kipindi cha miezi 12, hongereni sana.Katika hili tuendelee kuongeza kasi ya usajili na kuhimiza wanachama wapya wajiunge na Jumuiya yetu hivyo hivyo wajiunge na Chama chetu kwasababu hatuna mtaji mwingine wa kufafutatia ushindi wa Chama zaidi ya wanachama,mashabiki na wapenzi wa Chama chetu pamoja na wanachama na wapenzi wa Jumuiya zetu,”amesema Gavu.

Ameongeza kuwa wakiendelea kusajili wanachama wapya maaana yake watakuwa wameongeza mtaji wa ushindi wa Chama cha Mapinduzi, hivyo amemuomba Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na viongozi wengine wa jumuiya hiyo kuongeza kasi zaidi.

Akieleza zaidi Gavu amesema hivi karibuni wamemaliza uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini kabla ya uchaguzi huo kulikuwa na taasisi nyingi nje ya Mfumo wa Chama chao ambazo zilikuwa zinajinasibu na kujisifia kuwa wao ndio walikuwa wanafanya kazi ya kumsaidia Rais,kumsifia Rais , kumtangaza Rais lakini ulipofika wakati uchaguzi huo waliosimama kwa ajili ya kukinadi Chama hicho ni wao wenyewe.

“Hakuna taasisi ,hakuna chawa,hakuna kunguni bali tuliokwenda kwenda kusimama,kukinadi na kukipigania Chama chetu tulikuwa ni sisi wana CCM na Jumuiya zetu.Kwahiyo Mwenyekiti wa Jumuiya UWT nataka msimame  kwa miguu miwilii …

“Mjipige kifua na muwathibitishie watanzania kwamba Chama chetu hakina shida ya watu wa kupiga debe , Chama chetu kipo kamilifu kina muundo thabiti, Jumuiya na wanachama tathibiti na sisi tumeamua kama tulivyoshinda katika Serikali za Mitaa,ushindi huo huo tutashinda katika uchaguzi Mkuu mwaka 2025

“Tunachokiomba wale wanachama,mashabiki na wapenzi wanaohitaji kutengeneza taasisi ama Vikundi au mikusanyiko yao kwa ajili ya kutusaidia kazi wasikilize miongozo na taratibu zitakazotolewa na Chama Cha Mapinduzi

 

 

The post Gavu ataka kasi zaidi kuongeza wanachama jumuiya za chama first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/LdFlZji
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Gavu ataka kasi zaidi kuongeza wanachama jumuiya za chama
Gavu ataka kasi zaidi kuongeza wanachama jumuiya za chama
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/12/IMG-20241217-WA0002-950x632.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/gavu-ataka-kasi-zaidi-kuongeza.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/gavu-ataka-kasi-zaidi-kuongeza.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy