Waziri Aweso avalia njuga suala la upatikanaji wa maji Dodoma
HomeHabariTop Stories

Waziri Aweso avalia njuga suala la upatikanaji wa maji Dodoma

Waziri wa Maji *Mh. Jumaa Aweso* jana amefanya ziara katika maeneo ya Miganga-Mkonze na Nkuhungu kuangalia hali ya upatikanaji wa maji Jijin...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo August 3, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo July 3, 2024
Picha mbalimbali za Uzinduzi wa Treni mpya ya kisasa SGR

Waziri wa Maji *Mh. Jumaa Aweso* jana amefanya ziara katika maeneo ya Miganga-Mkonze na Nkuhungu kuangalia hali ya upatikanaji wa maji Jijini Dodoma na kutoa maelekezo kwa watendaji maji kuimarisha utafiti wa kina wa upatikanaji wa maji ili zoezi la uchimbaji visima virefu lianze kwa uharaka.

 

“Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan ametupatia vifaa vya kisasa vya utafiti wa kina wa upatikanaji wa maji,nataka vianze kazi hiyo hapa Jijini Dodoma ili tuendelee na uchimbaji wa visima virefu kutatua adha ya upatikanaji wa maji iliyosababishwa na ongezeko kubwa la watu Jijini Dodoma.

 

Wakati tunasubiri mradi mkubwa wa kutoa maji Ziwa Victoria na Mradi wa Bwawa la Farkwa,endeleeni kuchimba visima virefu maeneo tofauti tofauti ya Jiji ili kupunguza adha ya maji hapa Dodoma.

 

Hakikisheni hamuwabambikizii wananchi bili za maji ni marufuku mtumishi wa mamlaka kufanya hivyo,ili kuondokana na changamoto kubwa iliyolalamikiwa ya kubambikiziwa bili ya maji,tunajiandaa kuja na mfumo wa kulipa maji kadri utakavyotumia“ Alisema Mh Aweso

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh. Anthony Mavunde* amemshukuru Waziri Aweso

Kwa jitahada kubwa za utatuzi wa kero ya maji Jijini Dodoma na kuomba rasmi utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa maji wa Nzuguni A ambao utasaidia upatikanaji wa maji katika maeneo ya Ihumwa,Nzuguni,Ilazo,Mlimwa C,Kisasa,Mailimbili,Area C,Area D na Chamwino ili sasa maji yaliyokuwa yakielekezwa maeneo hayo yabadilishwe muelekeo kuwahudumia wananchi ambao awali mgawo wao wa maji ulikuwa mkubwa.

 

Akitia taarifa yake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA) *Mhandisi Aron Joseph* amesema mahitaji ya maji Jijini Dodoma kwa siku ni lita Milioni 147 na huku uzalishaji wa maji ni lita Milioni 79 na hivyo kuwa na upungufu wa lita 68m kwa usiku hali inayopelekea mgao mkubwa wa maji.

The post Waziri Aweso avalia njuga suala la upatikanaji wa maji Dodoma first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/btHLFId
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Aweso avalia njuga suala la upatikanaji wa maji Dodoma
Waziri Aweso avalia njuga suala la upatikanaji wa maji Dodoma
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/11/IMG-20241101-WA0009-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/waziri-aweso-avalia-njuga-suala-la.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/waziri-aweso-avalia-njuga-suala-la.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy