NYOTA wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, Haruna Niyonzima mkataba wake unameguka pale msimu utakapoisha wa...
NYOTA wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, Haruna Niyonzima mkataba wake unameguka pale msimu utakapoisha wa 2020/21 kwa kuwa awali aliongeza kandarasi ya miezi sita.
Uongozi wa Yanga umempa mkongwe huyo heshima kwa kumuaga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu FC ambao unatarajiwa kuchezwa Julai 15 Uwanja wa Mkapa.
Taarifa kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram ya Yanga imeeleza kuwa Julai 15 itakuwa ni Niyonzima Day na kuwaomba mashabiki waikose siku hiyo.
Kiungo huyo amecheza kwa muda mrefu ndani ya Yanga pia aliwahi kucheza kwa watan zai wa jadi Simba na aliweza kuwa miongoni mwa wachezaji waliotinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa huko.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS