DC Magoti aahidi kuendeleza na kutunza miundombinu ya unawaji mikono iliyojengwa na Shirika la Water Aid Kisarawe
HomeHabariTop Stories

DC Magoti aahidi kuendeleza na kutunza miundombinu ya unawaji mikono iliyojengwa na Shirika la Water Aid Kisarawe

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Peter Magoti, ameahidi kuendeleza na kutunza miundombinu ya unawaji mikono iliyojengwa na Shirika la Water Aid k...

Bayern wanataka kumnunua Colwill wa Chelsea huku Kompany akionekana kuimarisha safu yake ya ulinzi.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 11, 2024
Ubalozi wa Tanzania Nigeria waendesha jukwaa kuvutia uwekezaji nchini

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Peter Magoti, ameahidi kuendeleza na kutunza miundombinu ya unawaji mikono iliyojengwa na Shirika la Water Aid katika uhamasishaji wa watu kunawa mikono.

Magoti aliyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya kunawa mikono iliyofanyika katika shule ya Msingi Kazumzumbwi Wilayani ya Kisarawe ambapo siku hii huadhimishwa ifikapo Oktoba 15, duniani kote.

Aidha, alisema siku ya kunawa mikono ni muhimu katika kutoa elimu kwa jamii ukizingatia mkono ndio kila kiti na itawaepusha na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya tumbo, macho, kichocho, kipindupindu, kuhara na magonjwa ya homa ya tumbo.

Kampeni ya kunawa mikono iliyoanzishwa na Shirika la Water Aid imefanya pia mambo mengi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya vyoo na kunawa mikono katika shule 30 na vituo 15 vya afya hivyo hawana budi kuvitunza ili viwasaidie kulinda afya za wanamchi na wanafunzi.

Naye Kaimu Mkurugeziwa wa Shirika la WaterAid, Christina Mhando, alisema lengo kuu la mradi wa unawaji mikono ni kuhamasisha tabia siha kwa wananfunzi na watoa huduma za afya walimu na jamii kwa ujumla.

Alisema huwa wanatumia siku hiyo kuwashawishi watunga sera watoa maamuzi, wafadhili na wadau mbalimbali umuhimu wa kuwekeza kwenye maji na usafi wa vyoo na kunawa.

“Tunatoa wito kwa jamii kuona umuhimu wa kunawa mikono kwa jamii kujikinga na magonjwa na kwa watoa huduma kuwakinga wale wanaowahudumia,”alisema

Naye Junita Maiko mwanafunzi wa shule ya Msingi Sungwi alisema katika maadhimisho hayo amejifunza mambo mbalimbali kubwa umuhimu wa unawaji mikono huku akiahidi kwenda kuwa balozi mzuri kwa jamii inayomzunguka.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Sungwi, Shabani Dude, alisema mradi huo umewasaidia hususani katika kuwajengea miundombinu.

Dude aliitaka jamii ielewe kwamba ukipata magonjwa kutokana na kutonawa mikono,wazazi watashindwa kuwalea watoto,watoto watashindwa kupata elimu na kwa ujumla taifa litashindwa kupata maendeleo.

 

The post DC Magoti aahidi kuendeleza na kutunza miundombinu ya unawaji mikono iliyojengwa na Shirika la Water Aid Kisarawe first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/qUhTQNa
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: DC Magoti aahidi kuendeleza na kutunza miundombinu ya unawaji mikono iliyojengwa na Shirika la Water Aid Kisarawe
DC Magoti aahidi kuendeleza na kutunza miundombinu ya unawaji mikono iliyojengwa na Shirika la Water Aid Kisarawe
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/10/IMG-20241015-WA0094-950x632.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/10/dc-magoti-aahidi-kuendeleza-na-kutunza.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/10/dc-magoti-aahidi-kuendeleza-na-kutunza.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy