Ziara ya Dkt Samia yavuna wapinzani Morogoro,abood awapokea
HomeHabariTop Stories

Ziara ya Dkt Samia yavuna wapinzani Morogoro,abood awapokea

Ikiwa ni siku chache Mkuu wa Nchi Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya Ziara kubwa ya Siku 6 Mkoani Morogoro kukutana na Wananchi, kuzindua Mira...

MSD yatakiwa kusimamia uendeshaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 20, 2025
Naibu waziri Kapinga awataka Pura kuongeza juhudi 

Ikiwa ni siku chache Mkuu wa Nchi Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya Ziara kubwa ya Siku 6 Mkoani Morogoro kukutana na Wananchi, kuzindua Miradi mikubwa ya Maendeleo ikiwemo ya Viwanda, Madaraja, Barabara, maabara mtambuka, Majengo ya Chuo Kikuu Mzumbe n.k, Wapinzani Morogoro Mjini wameshindwa kuvumilia na kuamua kuamia Chama cha Mapinduzi.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abood amepokea wanachama wapya kutoka Vyama mbalimbali vya Upinzani walioamua kwa hiari yao kujiunga na CCM mara baada ya kuridhishwa na Kazi nzuri inayofanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mapokezi hayo yamefanywa tarehe Katika Soko kubwa la Matunda na Mbogamboga (Soko la Mawenzi) wakati akizindua Shina walioanzisha wao la Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi Mawenzi Sokoni.

Akizungumza nao, Mhe. Mbunge amewakaribisha kwa mikono miwili na kuwapongeza kwa maamuzi yao mazuri ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi uku akikubaliana nao kuwa Mhe. Dkt. Samia amefanya kazi kubwa Nchini na anaendelea kufanya kwa kishindo kikubwa kuwaletea Watanzania Maendeo, sambamba na hilo Mhe. Mbunge ameeleza upendo Mkubwa wa Dkt. Samia na kusema

“Mmeshuhudia Juzi Mhe. Rais alikuja Morogoro kututembelea, tumezungumza shida zetu na papohapo akazitatua, tumeomba hospitali ya rufaa katumwagia Bilion 5 palepale, tumemuomba maji mkataba wa bilioni 185 umecheleweshwa kusainiwa kamuelekeza Waziri mpaka oktaba mkataba usainiwe, tumemuomba pesa za barabara, amemuelekeza Waziri atuongezee, hivyo tuna kila sababu ya kumshukuru Rais wetu na ndio maana leo wenzetu uvumilivu umewashinda”.*

Aidha Mhe. Mbunge amewapongeza Wafanyabiara wa soko la Mawenzi kwa umoja wao na shughuli kubwa na nzuri wanayoifanya ya kulisha Morogoro na kushiriki katika ujenzi wa Nchi yao, vilevile ameahidi kuendelea kutatua kero na changamoto za soko hilo uku akibainisha alivyochonga barabara za soko hilo zilizokuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara hao na kueleza mafanikio waliyoyapata baada ya kupata eneo hilo kutoka posta mpaka manispaa na sasa soko la kisasa labidi kujengwa.

Nae Katibu wa idara ya Uenezi Morogoro Mjini Ndugu Maulid Chamilila amewakaribisha kwa kishindo kikubwa wanachama wapya kutoka upinzani uku Diwani wa Kata hiyo Mhe Mbuguyu akieleza mafanikio yaliyofikiwa kwenye kata hiyo ikiwemo ujenzi wa Zahana n.k

Wanachama hao wapya kutoka katika vyama vya upinzani wameeleza furaha yao kujiunga CCM hasa wakielekeza shukurani zao kwa Mhe. Rais kwa kazi nzuri aliyoifanya na kuendelea kuifanya Nchini Kote.

The post Ziara ya Dkt Samia yavuna wapinzani Morogoro,abood awapokea first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/8gy3oUH
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Ziara ya Dkt Samia yavuna wapinzani Morogoro,abood awapokea
Ziara ya Dkt Samia yavuna wapinzani Morogoro,abood awapokea
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/08/16d975f8-4b0b-445d-9790-b84e4ce8e9f0-950x633.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/ziara-ya-dkt-samia-yavuna-wapinzani.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/ziara-ya-dkt-samia-yavuna-wapinzani.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy