Waziri Ummy:Ugonjwa Usiojulikana Mkoa Wa Lindi Ni Homa Ya Mgunda
HomeHabari

Waziri Ummy:Ugonjwa Usiojulikana Mkoa Wa Lindi Ni Homa Ya Mgunda

Na Englibert Kayombo,WAF,Ruangwa Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema kuwa upimaji wa sampuli za wagonjwa waliokuwa wakiugua Ug...

Kilimo Hai Ni Ajira Ya Uhakika Kwa Vijana
Wabunge wataka wazee wa mabaraza kuongezewa posho
Rais Samia Suluhu Hassan Ahudhuria Kikao Cha Kamati Kuu Ya CCM Jijini Dodoma Leo

Na Englibert Kayombo,WAF,Ruangwa

Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema kuwa upimaji wa sampuli za wagonjwa waliokuwa wakiugua Ugonjwa Usiojulikana katika Wilaya ya Ruangwa katika Mkoa wa Lindi umethibitisha mlipuko huu kuwa wa ugonjwa wa Leptospirosis, Field Fever kwa lugha ya Kiswahili inajulikana kama Homa ya Mgunda.

Waziri Ummy amesema hayo  mara baada ya kutembelea Wilaya ya Ruangwa katika Mkoa wa Lindi ambako kumezuka Mlipuko wa Ugonjwa huo na kuzungumza na Waandishi wa Habari.

Waziri Ummy amesema kuwa Homa ya Mgunda ni miongoni mwa magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu na unasababishwa na Bakteria aina ya Leptospira interrogans.

“Ugonjwa huu umekuwepo katika maeneo ya kitropiki ambayo ni yenye hali ya joto katika mabara ya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Afrika, Asia na Australia. Wanyama aina za panya, kindi, mbweha, kulungu, swala, na wanyamapori wengine wameripotiwa kupata maambukizi ya vimelea hivi na kuwa chanzo cha maambukizi kwa binadamu” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Amesema kuwa Ugonjwa wa Homa ya Mgunda huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia uchafuzi wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji kutoka katika mkojo wa wanyama wenye maambukizi.

Waziri Ummy amesema mtu anaweza kupata ugonjwa huo kwa Kugusa mkojo (au maji maji mengine ya mwili) kutoka kwa wanyama wenye maambukizi; Kugusa maji, udongo, au chakula kilichochafuliwa na mkojo wa wanyama wenye maambukizi au kunywa maji yaliyochafuliwa na vimelea vya bakteria wa ugonjwa huo huku maambukizi ya ugonjwa huu kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine hutokea kwa nadra.

Waziri Ummy amewataka kuchukua hatua zote stahiki za kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuepuka kugusa maji au vitu vilivyochafuliwa na mkojo wa wanyama na kunywa maji safi na salama ambayo yamechemshwa au kutibiwa pamoja na kuwataka wagonjwa wenye dalili za homa, kuvuja damu, kichwa kuuma na mwili kuchoka kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wapate matibabu sahihi

“Wizara inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huu na kuendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu. Hivyo Serikali inawaasa Wananchi kutokuwa na hofu kwani ugonjwa huu unaendelea kudhibitiwa” amesema Waziri Ummy Mwalimuj




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Ummy:Ugonjwa Usiojulikana Mkoa Wa Lindi Ni Homa Ya Mgunda
Waziri Ummy:Ugonjwa Usiojulikana Mkoa Wa Lindi Ni Homa Ya Mgunda
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhskjodMhK0sRmPcn_jZ2p3yumQP3dW8wtdabfaoGzatxIM-iYd9sTkLrAfDy4v-FYVuWGTekcatVoxd95F86_tMvw2oAelzN-bn8HNCv6tzy7VhqcvWwRLfGlORHYzz_I-isXu9i0c272uax9ipx1azfqVYi90Gs9Pc8xAbc4b8ZJ6x2mlmbrWCr7s9A/s16000/69c301ee-ae8d-408a-955c-67fdeb6f2858-1024x700.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhskjodMhK0sRmPcn_jZ2p3yumQP3dW8wtdabfaoGzatxIM-iYd9sTkLrAfDy4v-FYVuWGTekcatVoxd95F86_tMvw2oAelzN-bn8HNCv6tzy7VhqcvWwRLfGlORHYzz_I-isXu9i0c272uax9ipx1azfqVYi90Gs9Pc8xAbc4b8ZJ6x2mlmbrWCr7s9A/s72-c/69c301ee-ae8d-408a-955c-67fdeb6f2858-1024x700.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/waziri-ummyugonjwa-usiojulikana-mkoa-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/waziri-ummyugonjwa-usiojulikana-mkoa-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy