Makamu Wa Rais Afungua Mkutano Wa Sayansi Wa NIMR
HomeHabari

Makamu Wa Rais Afungua Mkutano Wa Sayansi Wa NIMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 17 Mei 2022 amefungua mkutano wa 31 wa pamoja ...

Ajali mbaya ya gari Njombe yaua watu wanne na kujeruhi 19
Bunge laahirishwa kupisha maombolezo ya Mbunge Irene Ndyamkama
Waziri Mkuu Awataka Watanzania Kutumia Fursa Za Muungano


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 17 Mei 2022 amefungua mkutano wa 31 wa pamoja wa Sayansi ulioandaliwa na  Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) unaofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Mkutano huo unashirikisha wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza na washiriki wa mkutano huo Amesema Tanzania inaunga mkono na kuamini katika ufanyaji wa tafiti zitakazokabiliana na changamoto za maradhi hapa nchini. Ameongeza kwamba mkutano huo ni fursa ya aina yake kwa wanasayansi wa Tanzania  kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuunganisha werevu na uwezo katika kupata masuluhisho ya kimsingi kwa changamoto kuu za kiafya hapa nchini.

Makamu wa Rais amesema mkutano huo una umuhimu mkubwa kutokana na kufanyika katika kipindi ambacho dunia, Tanzania ikiwemo inapitia katika changamoto mbalimbali za magonjwa kama vile Uviko 19 pamoja na magonjwa yasioambukiza. Aidha ameongeza kwamba serikali imedhamiria kufikisha huduma za kiafya katika maeneo yote hapa nchini na itaendelea kushirikiana na wadau wote wakiwemo watafiti na sekta binafsi.

Halikadhalika Makamu wa Rais ameiagiza Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) kuongeza kasi ya ufanyaji utafiti pamoja na kuzalisha chanjo na dawa bora za asili.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wizara itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ili kuweza kutumiza majukumu yao kwa ufanisi. Amesema tayari NIMR imeshiriki katika tafiti mbalimbali zinazowezesha katika utungaji wa sera na mipango katika wizara ya afya ikiwemo kuwezesha Wizara kupata uhalisia wa utoaji wa chanjo ya HPV ambayo inakinga wasichana dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Makamu Wa Rais Afungua Mkutano Wa Sayansi Wa NIMR
Makamu Wa Rais Afungua Mkutano Wa Sayansi Wa NIMR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJ_u2FeIKOqzH6AITw85WOyq1KmhAc3Lnk-t5pMqIqePUrclkSnX_mickWz-8YhbiNz1c8DPXYziqeCV7M-1xBGW1Gs802yOSlxSlMjPVkdFTA4DdpLrz1la1oYwRGQu05aqODNMB7XG4epa5dWvbzJ9pciKrZHVSz-8KQVndThpR4cb_rrT6QKF28qw/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJ_u2FeIKOqzH6AITw85WOyq1KmhAc3Lnk-t5pMqIqePUrclkSnX_mickWz-8YhbiNz1c8DPXYziqeCV7M-1xBGW1Gs802yOSlxSlMjPVkdFTA4DdpLrz1la1oYwRGQu05aqODNMB7XG4epa5dWvbzJ9pciKrZHVSz-8KQVndThpR4cb_rrT6QKF28qw/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy