Rais Mwinyi Atangaza Siku 7 Za Maombolezo Zanzibar Kufuatia Kifo Cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
HomeHabari

Rais Mwinyi Atangaza Siku 7 Za Maombolezo Zanzibar Kufuatia Kifo Cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  ametangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera zitapepe...

Waziri Ummy Atoa Maamuzi Magumu Ujenzi Wa Makao Makuu Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo August 12
Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo Atoa Siku 14 Kwa Viongozi Ngazi Ya Wilaya Na Mikoa Kukagua Utekelezaji Wa Ilani Na Taarifa Iwasilishwe Ofisini Kwake


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  ametangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kilichotokea jana Februari 2021 mnamo majira ya saa 5:26 asubuhi.


Akitangaza kutokea kwa msiba huo, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki dunia wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar-es-Salaam ambako alikuwa amelazwa tokea tarehe 09 Februari, 2021.


“Kwa niaba ya wananchi, nachukua fursa hii kutoa pole na salamu zangu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, Chama cha ACT-Wazalendo na wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania na kuwataka wawe na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki cha majonzi”, alisema Rais Dk. Mwinyi katika taarifa hiyo.


Aidha, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa hakika Taifa limepoteza kiongozi Mzalendo na shupavu.


Sambamba na hayo, Rais Dk. Mwinyi katika taarifa hiyo maalum ya tanzia alieleza kuwa taarifa zaidi za msiba huo na maziko yake zitaendelea kutolewa na Serikali kwa ushirikiano wa karibu na familia pamoja na chama cha ACT-Wazalendo.


Rais Dk. Mwinyi alimuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi. Amin.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Mwinyi Atangaza Siku 7 Za Maombolezo Zanzibar Kufuatia Kifo Cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
Rais Mwinyi Atangaza Siku 7 Za Maombolezo Zanzibar Kufuatia Kifo Cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtoZIf5dcBOjQOBImimHBBri4Rrf7JkmERMDZyOrH1YtXvS7AF5T94IqNvaZ9vlN0MpgYoEViHilRvjrf8BXIOV25_sskSwCqgTNjMJ45gACZM7-DqPyW-CrCN2mm9zqQR2VMEtJ6vSB7S/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtoZIf5dcBOjQOBImimHBBri4Rrf7JkmERMDZyOrH1YtXvS7AF5T94IqNvaZ9vlN0MpgYoEViHilRvjrf8BXIOV25_sskSwCqgTNjMJ45gACZM7-DqPyW-CrCN2mm9zqQR2VMEtJ6vSB7S/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/rais-mwinyi-atangaza-siku-7-za.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/rais-mwinyi-atangaza-siku-7-za.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy