Waziri Ummy Ataka Hospitali Ya Mloganzila Kuanza Kujitegemea
HomeHabari

Waziri Ummy Ataka Hospitali Ya Mloganzila Kuanza Kujitegemea

Na. WAF – Dar es Salaam Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kufikia Julai Mosi 2022 Hospitali ya Mlonganzila ianze kujitegemea yeny...

Kamati tatu za Bunge zamgomea Makinda
Wakerwa shilingi kushuka thamani
Watafiti UDSM kusafisha majitaka kuwa ya kunywa


Na. WAF – Dar es Salaam
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kufikia Julai Mosi 2022 Hospitali ya Mlonganzila ianze kujitegemea yenyewe badala ya kuendelea kuwa chini ya Bodi ya wakurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili.

Waziri Ummy amesema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Hospitali ya Mloganzila wakiwemo wakurugenzi na viongozi waandamizi mara baada ya kuzindua miradi ya mtambo wa kuzalisha hewa tiba (Oxygen generating plant) pamoja na mradi wa kuboresha huduma ya mama na mtoto ambao umelenga kukarabati wodi ya watoto wachanga mahututi (Neonatal ICU).

“Hospital hii imekuwa chini ya Bodi ya wakurugenzi wa hospitali ya Muhimbili kwa muda wa miaka minne sasa inatosha ikajitegemee yenyewe, ijisimamie kwa kujiendesha na kutoa huduma za matibabu kwa wananchi”. Amesema Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa atahakikisha mchakato wa Hospitali hiyo kujitegemea unaharakishwa ili usiweze kukwamisha ifikapo Julai mosi.

Kwa upande wa uzinduzi wa miradi, Waziri Ummy amesema Mradi wa hewa tiba ya Oksijeni utasaidia kuzalisha mitungi 200 kwa siku na mradi wa pili umelenga kukarabati wodi ya watoto wachanga mahututi (Neonatal ICU) kwa msaada wa Serikali ya Korea.

Aidha, Waziri Ummy amebainisha kuwa Serikali imeamua kuanza kufanya uwekezaji kwa kusimika mitambo ya uzalishaji wa gesi tiba baada ya kuona changamoto za upatikanaji wake pamoja na gharama kuwa kubwa.

“Mwaka 2021 tumefanikiwa kufunga mitambo Saba katika Hospitali za Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Amana, Geita, Mbeya, Manyara na Dodoma ambayo imeunganishwa moja kwa moja mpaka wodini aliko mgonjwa”. Amesema Waziri Ummy

Hata hivyo Waziri Ummy amesema Serikali ipo mbioni kukamilisha awamu ya pili ya ununuzi wa mitambo hiyo katika Mikoa kumi na mbili (12) kwa hospital za Rufaa ikiwemo Njombe, Songwe, Rukwa, Tabora, Kigoma, Mara, Simiyu, Morogoro Sokoine, Shinyanga, Katavi na Sekoe Toure.

Kwa upande wake Balozi wa Korea nchini Tanzania Mhe. Kim Sun Pyo amesema nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania hasa katika sekta ya Afya na kuahidi kusaidia katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.

“Nchi ya Tanzania na Korea ilianza ushirikiano muda mrefu toka miaka ya 1992 kwa kusaidiana katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya na tutaendelea kufanya hivyo”. Amesema Balozi Kim.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Ummy Ataka Hospitali Ya Mloganzila Kuanza Kujitegemea
Waziri Ummy Ataka Hospitali Ya Mloganzila Kuanza Kujitegemea
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgn5sEkHVaQfwD7p0-F7GTZFHpHAVKAO2uH5aFohbQfdZsU--Odklyw6cuc8LwBWQaulFTEe7vfwVI0ReJN4oiQFEr1dgj21Y9B5QxpQxYgVnBxKntqX4a5hHvcOW4F7iZ_FTmquHm0KufJsqmDPxoLlRoQJYrEPv7kMLCentUpCqs1BEQs6tzBiutFzw/s16000/1.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgn5sEkHVaQfwD7p0-F7GTZFHpHAVKAO2uH5aFohbQfdZsU--Odklyw6cuc8LwBWQaulFTEe7vfwVI0ReJN4oiQFEr1dgj21Y9B5QxpQxYgVnBxKntqX4a5hHvcOW4F7iZ_FTmquHm0KufJsqmDPxoLlRoQJYrEPv7kMLCentUpCqs1BEQs6tzBiutFzw/s72-c/1.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/waziri-ummy-ataka-hospitali-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/waziri-ummy-ataka-hospitali-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy