Waziri Kijaji:serikali Itaendelea Kuliwezesha Shirika La NDC
HomeHabari

Waziri Kijaji:serikali Itaendelea Kuliwezesha Shirika La NDC

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji  amesema Serikali itaendelea kuliwezesha Shirika la Taifa la Maendeleo (...


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji  amesema Serikali itaendelea kuliwezesha Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa kishirikiana na Taasisi nyingine za umma katika uzalishaji na usambazaji wa viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa malaria ili kutokomeza ugonjwa huo nchini.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati  wa utoaji wa Taarifa  ya  Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza  viluwiluwi waenezao ugonjwa wa malaria (Tanzania Biotech Products – TBPL)  kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Februari 4, 2022  katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo (Mb) amesema Kamati hiyo imedhamiria kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini na iko tayali kushirikiana na Wizara  kuona Shirika hilo linafanya kazi kwa ufanisi katika kuzalisha viuadudu hivyo na  kusambaza nchi nzima ili kuokoa maisha ya watanzania wengi.

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali  yanayolenga kuboresha uzalishaji na kuweka utaratibu mzuri wa ununuzi na usambazaji wa viuwadudu vinanvyouwa viluwiluwi wa mbu waenezao malaria ili kutokomeza malaria nchini katika kipindi kitakachopangwa .

Awali, akitoa taarifa hiyo ya Kiwanda cha TBPL kwa wajumbe wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Dkt. Nicholas Shombe amesema Serikali imeanzisha Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza  viluwiluwi vya mbu waenezao Malaria na magonjwa mengine Dengue, Zika, Chikungunya, Matende na Mabusha ili kutokomeza magojwa hayo nchini.

Kiwanda hiki  cha TBPL kilichopo mkoani Pwani, kinamilikiwa na Serikali kwa 100% chini ya NDC na  una uwezo wa kuzalisha Viuadudu  vya kuua viluwiluwi wa mbu,
viuatilifu vya kibalojia ( bio – pestcides) kwa ajili ya kuua wadudu wadhurifu katika mazao ya pamba na mbogamboga na  mbolea (bio – fertilizer). Kwa mujibu watakwimu za NBS 2020,  Dawa hizi viuadudu zimechangia kushuka kwa maambukizi ya malaria nchini kutoa asolkmia 14 hadi 7.3. Amesema Dkt. Nicholas Shombe.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Kijaji:serikali Itaendelea Kuliwezesha Shirika La NDC
Waziri Kijaji:serikali Itaendelea Kuliwezesha Shirika La NDC
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgKWI2olMC1kZvQRuWujebzwfmRiSMeB-PEIHznZyJLb_a2JslUrYoiQW27vR_kgM0D5Ge365r7pi9AYcWiVFfqdb-yYpCuzRYvE-ugiqs3c2HY757P5RdG_7PS7npwpeP94ORlKpocEY801tz0VJFNsj6C34OsgUx7rReyG3e6WV4YDUvBF-j7Px2TLQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgKWI2olMC1kZvQRuWujebzwfmRiSMeB-PEIHznZyJLb_a2JslUrYoiQW27vR_kgM0D5Ge365r7pi9AYcWiVFfqdb-yYpCuzRYvE-ugiqs3c2HY757P5RdG_7PS7npwpeP94ORlKpocEY801tz0VJFNsj6C34OsgUx7rReyG3e6WV4YDUvBF-j7Px2TLQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/waziri-kijajiserikali-itaendelea.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/waziri-kijajiserikali-itaendelea.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy