Mafunzo Ya Pamoja Ya Kijeshi Yaimarisha Ushirikiano Wa Kiusalama Kati Ya Marekani Na Tanzania.
HomeHabari

Mafunzo Ya Pamoja Ya Kijeshi Yaimarisha Ushirikiano Wa Kiusalama Kati Ya Marekani Na Tanzania.

Askari wa vikosi maalumu vya majeshi ya Marekani na Tanzania leo wamemaliza mafunzo ya pamoja (Joint Combined Exchange Training – JCET) ya...

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 29, 2024
Rais wa Yanga SC akabidhiwa rasmi ofisi
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 28, 2024

Askari wa vikosi maalumu vya majeshi ya Marekani na Tanzania leo wamemaliza mafunzo ya pamoja (Joint Combined Exchange Training – JCET) ya wiki nane, wakipiga hatua nyingine katika historia ya ushirikiano wa kiusalama kati ya nchi hizi mbili.

Rear Admiral Ramson Godwin Mwaisaka, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji Tanzania, aliongoza hafla ya kufungwa kwa mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Oparesheni za Kulinda Amani, Kunduchi, Dar es Salaam. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mwambata Mwandamizi wa Kijeshi katika Ubalozi wa Marekani, Luteni Kanali Serge Mettes na askari kutoka Kikosi cha Oparesheni Maalumu cha Jeshi la Marekani, Kamandi ya Afrika.

“Tanzania ni kiongozi katika kuhakikisha amani na utulivu katika kanda na tunashukuru kuwa na ubia imara na nchi hii katika masuala ya usalama. Majeshi yetu yana historia ya muda mrefu ya kufanya kazi bega kwa bega na mafunzo haya yaliandaliwa maalumu kuboresha zaidi uwezo wa kufanya kazi pamoja na kuzifanya oparesheni za pamoja kuwa imara zaidi,” alisema Mettes.

Mafunzo haya yaliwaleta pamoja askari wa Vikosi Maalumu vya Jeshi la Marekani na wale wa Vikosi Maalumu vya Wanamaji wa Tanzania katika mafunzo ya wiki nane, wakijifunza pamoja stadi mbalimbali za kijeshi kama vile mbinu za uendeshaji wa kikundi kidogo cha askari, kulenga shabaha, huduma za matibabu, mbinu za medani, Sheria za Migogoro ya Kivita na ulinzi wa haki za binadamu wakati wa vita.

Haya yalikuwa mafunzo ya pili ya pamoja kati ya majeshi ya Marekani na Tanzania katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.  Kwa mujibu wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright, kufanyika mara kwa mara kwa mafunzo na mazoezi haya ya pamoja ni kielelezo cha umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano imara wa kiusalama baina yake na Tanzania.

“Ushirikiano katika nyanja ya usalama ni nguzo ya ushirikiano rasmi kati ya Marekani na Tanzania. Ubia wetu wa miaka 60 umejengwa katika maadili ya pamoja na kuheshimiana, na unaendelea kuimarika siku hadi siku,” alisema Balozi Wright.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mafunzo Ya Pamoja Ya Kijeshi Yaimarisha Ushirikiano Wa Kiusalama Kati Ya Marekani Na Tanzania.
Mafunzo Ya Pamoja Ya Kijeshi Yaimarisha Ushirikiano Wa Kiusalama Kati Ya Marekani Na Tanzania.
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgIBWdctd8skyRa3p_lOgSyi0hGdto7RTqs2dvVneMYBNXOhQcMjLGaDU0QRdXHrcGmzsHb6fwVSHxE3QTGiEvMdNz2tIQDlJmkbHbt4STYa0Ua0-MnJT3-KOfBuebQSkamuuxd6s5DRvE-UEZJHRkfGkiqJMQMsei_B1fxGfFYtOlUBsaJtPtDKPrq3A=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgIBWdctd8skyRa3p_lOgSyi0hGdto7RTqs2dvVneMYBNXOhQcMjLGaDU0QRdXHrcGmzsHb6fwVSHxE3QTGiEvMdNz2tIQDlJmkbHbt4STYa0Ua0-MnJT3-KOfBuebQSkamuuxd6s5DRvE-UEZJHRkfGkiqJMQMsei_B1fxGfFYtOlUBsaJtPtDKPrq3A=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/mafunzo-ya-pamoja-ya-kijeshi-yaimarisha.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/mafunzo-ya-pamoja-ya-kijeshi-yaimarisha.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy