Wasambazaji Wa Bidhaa Za Vifaa Vya Ujenzi Waonywa Kupandisha Bei Bila Sababu Za Msingi
HomeHabari

Wasambazaji Wa Bidhaa Za Vifaa Vya Ujenzi Waonywa Kupandisha Bei Bila Sababu Za Msingi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amewaonyza wasambazaji wa bidhaa za vifaa vya ujenzi kutok...

Maafisa, Askari 14 Wa Tawa Wavishwa Vyeo Vipya Vya Jeshi La Uhifadhimaafisa, Askari 14 Wa Tawa Wavishwa Vyeo Vipya Vya Jeshi La Uhifadhi
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Disemba 19
Serikali Itaendelea Kuunga Mkono Juhudi Za Mashirika Yasiyokuwa Ya Kiserikali (Ngos)


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amewaonyza wasambazaji wa bidhaa za vifaa vya ujenzi kutokupandisha bei kwakuwa ni kosa la kisheria kupandisha bei za bidhaa hizo bila sababu ya msingi.

Prof. Kahyarara ameyasema hayo alipokutana na kuongea na wasambazaji wa bidhaa za vifaa vya ujenzi Dodoma, Februari 3, 2022 kuhusu sababu za  upandishaji wa bei na kupokea maoni ya jinsi ya kukabiliana na suala hilo ili kukuza biashara na kuwalinda walaji na  kutimiza  lengo la Serikali katika kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya taifa na wananchi.

Aidha, Katibu Mkuu huyo, aliwashauri wafanyabiashara na wasambazaji hao kujiandaa na kufanya biashara kwa ushindani pamoja na kuchangamkia fursa za Mkataba wa Kuanzisha Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) ambao Tanzania imeridhia na kujiunga. Mkataba huo unalenga kuwezesha uwekezaji na ufanyaji biashara baina ya nchi na nchi katika soko lenye watu takribani bilioni 1.3 linalotarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi, kibiashara na kijamii barani Afrika

Nao, Wasambazaji wa bidhaa za ujenzi hususan saruji, nondo na mabati jijini Dodoma, walipata fursa ya kutoa sababu zinazochangia kupanda kwa bei ya bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na  kununua bidhaa hizo kwa bei kubwa kutoka kwa wasambazaji wakubwa, gharama kubwa za usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka viwandani hadi maeneo yao husika pamoja na kupanda kwa bei ya malighafi za kutengenezea mabati kutoka nje ya nchi, bei kubwa ya kusafirisha malighafi hizo kutoka nje ya nchi.

Aidha, wakitoa mapendekezo mbalimbali ya jinsi ya kukabiliana na upandaji wa bei za vifaa vya ujenzi, Wasambazaji hao waliishauri Serikali kuanzisha mfumo  bei  elekezi ya saruji kulingana na maeneo waliopo kijiografia pamoja na kuwashauri wamiliki wa viwanda kuboresha mfumo wa usambazaji wa bidhaa kwa kuruhusu kuwa na wasambazaji wa bidhaa zao wengi badala ya kuwa na wasambazaji wakubwa wachache.

Akipokea maoni na mapendekezo hayo, Prof. Kahyarara  aliwapongeza  wasambazaji hao kwa maoni na mapendekezo yao muhimu na kuahidi kuyafanyia kazi huku akiwashauri kipunguza bei za bidhaa za vifaa vya ujenzi kuwa katika hali halisi bila kuwaumiza walaji wa mwisho ili kujenga uchumi imara.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wasambazaji Wa Bidhaa Za Vifaa Vya Ujenzi Waonywa Kupandisha Bei Bila Sababu Za Msingi
Wasambazaji Wa Bidhaa Za Vifaa Vya Ujenzi Waonywa Kupandisha Bei Bila Sababu Za Msingi
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEi5oLCMZOVZNtHdh5sKQRc0YrhYiDWCusVXSEnufPu29ZiiZ3i2Hy2WF68MZSzYjdgWu4udJu0SKBnhvg_fpxUXf0YOW6YAM6ICZHMQ0a7W_wpfQ9gxmfNEUYSEE2hVMqluouCnvMy2XYm_DdNsKcKbaSuiaLvwfdiJ1dhdV78O36Q0dG8TriqTN8Z0-Q=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEi5oLCMZOVZNtHdh5sKQRc0YrhYiDWCusVXSEnufPu29ZiiZ3i2Hy2WF68MZSzYjdgWu4udJu0SKBnhvg_fpxUXf0YOW6YAM6ICZHMQ0a7W_wpfQ9gxmfNEUYSEE2hVMqluouCnvMy2XYm_DdNsKcKbaSuiaLvwfdiJ1dhdV78O36Q0dG8TriqTN8Z0-Q=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/wasambazaji-wa-bidhaa-za-vifaa-vya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/wasambazaji-wa-bidhaa-za-vifaa-vya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy