Makamu Wa Rais Kuzindua Sera Ya Taifa Ya Mazingira
HomeHabari

Makamu Wa Rais Kuzindua Sera Ya Taifa Ya Mazingira

Makamu wa Rais Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ...

Dereva aliesababisha ajali iliyoua Polisi ahukumiwa miaka minne jela
Wachimbaji Madini Waaswa Kujikinga Dhidi Ya Maambukizi Ya Ukimwi- Waziri Biteko
Vijana Watakiwa Kujitokeza Kupima UKIMWI


Makamu wa Rais Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 inayotarijiwa kuzinduliwa 12 Februari, 2022 Jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dodoma  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga amesema Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 imejumuisha masuala ya mazingira yaliyokuwemo katika Sera ya 1997 na masuala mapya.

Ameyataja masuala mapya katika Sera mpya ya mwaka 2021 ni pamoja na: Udhibiti wa taka za kielektroniki, Usimamizi na matumizi ya kemikali, na Udhibiti wa uchafuzi katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi. Masuala mengine ni pamoja na Mabadiliko ya tabianchi; Usimamizi wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa; na Udhibiti wa viumbe vamizi.

“Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 imeongeza wigo wa masuala na changamoto za mazingira zinazopaswa kufanyiwa kazi katika kipindi husika ili kuleta maendeleo endelevu na imezingatia changamoto mpya za kimazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na mabadiliko ya mifumo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira yanayoendelea duniani” Alisisitiza Bi. Mary Maganga.

Amesema kuwa, Serikali imeamua kuwa na Wiki ya Uzinduzi wa Sera  itakayoanza tarehe 07-12/02/2022 ambayo itaambatana na shughuli mbalimbali za hifadhi ya mazingira ikiwa ni sehemu ya masuala ya msingi yanayoelekezwa katika Sera mpya.

Bi. Maganga amezitaja shughuli zitakazofanyika katika wiki hiyo kuwa ni Upandaji miti Jijini Dodoma katika maeneo ya Medeli, Iyumbu, Iseni na maeneo ya barabara inayoanzia Chimwaga, Chuo Kikuu cha Dodoma kuelekea barabara ya Dodoma Dar es Salaam. Aidha, Kufanya usafi pembezoni mwa barabara inayoanzia Shule ya Martin Luther hadi Wajenzi kupitia Nzuguni, Ilazo, Ipagala na Area C; Kutoa elimu kuhusu utenganishaji wa taka, kufanya Usafi katika soko la Changombe pamoja na Utoaji wa Elimu ya Mazingira kwa wananchi na wadau kupita vyombo vya habari.

Dhumuni la kuwepo kwa shughuli hizo ni kurejesha hali ya asili ya mazingira iliyoharibika kutokana na shughuli za kibinadamu kwa kuwa na zoezi la upandaji miti, kuboresha afya ya jamii na elimu ya utenganishaji taka kwa ajili ya udhibiti wa taka ngumu na kuwezesha urejelezaji wa taka kwenye bidhaa na huduma mbalimbali.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Makamu Wa Rais Kuzindua Sera Ya Taifa Ya Mazingira
Makamu Wa Rais Kuzindua Sera Ya Taifa Ya Mazingira
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhbnIRz2EHoDWlM0y04ruUEqfHNDhWCPE8BJBtgYjtRZkwLSOrQivQ-giq0MMXb9GWw2H2Mi6IOSx9bC0uA9fwSDYITOXf9a6aKFRP5gBX5iO6LYnfr01AKTi3N86LO6V1s_XsGyqkgPxfJ4sPGOUQ7Ic8lOZDhziGaAp2xVBMiT9LutUO74O6sX6DCgQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhbnIRz2EHoDWlM0y04ruUEqfHNDhWCPE8BJBtgYjtRZkwLSOrQivQ-giq0MMXb9GWw2H2Mi6IOSx9bC0uA9fwSDYITOXf9a6aKFRP5gBX5iO6LYnfr01AKTi3N86LO6V1s_XsGyqkgPxfJ4sPGOUQ7Ic8lOZDhziGaAp2xVBMiT9LutUO74O6sX6DCgQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/makamu-wa-rais-kuzindua-sera-ya-taifa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/makamu-wa-rais-kuzindua-sera-ya-taifa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy