Waziri Kikwete azindua miradi yenye thamani ya shilingi bil.1.6 wilayani Songwe
HomeHabariTop Stories

Waziri Kikwete azindua miradi yenye thamani ya shilingi bil.1.6 wilayani Songwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi , Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua miradi ya Elimu, Umeme na barab...

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi , Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua miradi ya Elimu, Umeme na barabara yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 katika Halmashauri ya wilaya ya Songwe mkoani Songwe

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Miradi hiyo leo tarehe 24 Februari 2025, amesema Mradi wa Ujenzi wa shule ya Maweni B ambao umegharimu shilingi milioni 583 utasaidia kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shule kwa watoto wa Mkwajuni, kupunguza msongamano darasani pamoja na utoro wa rejareja.

Mhe.Kikwete amezindua pia madarasa Sita yatakayotumika kwa kidato cha Tano na Sita katika shule ya sekondari Kanga. Mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 150 utawezesha pia vijana kuishi bweni na kuboresha mazingira ya malazi na Ujifunzaji kwa wanafunzi.

Amezindua ujenzi wa barabara za Mkwajuni mjini kwa Kiwango cha lami wenye thamani ya shilingi milioni 760, Mhe. Kikwete amempongeza Mbunge wa jimbo la Songwe, Mhe. Philipo Mulugo kwa kuelekeza kiasi cha shilingi Milioni 500 za mfuko wa maendeleo ya Jimbo kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kikwete amezindua Mradi wa usambazaji umeme Kitongoji cha Kikuyuni kata ya Mkwajuni wenye thamani ya shilingi milioni 156. Amesema, fedha hizo zimetolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa lengo la kuchochea maendeleo na ustawi wa watanzania hususani waishio vijijini.

The post Waziri Kikwete azindua miradi yenye thamani ya shilingi bil.1.6 wilayani Songwe first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/yAhiK48
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Kikwete azindua miradi yenye thamani ya shilingi bil.1.6 wilayani Songwe
Waziri Kikwete azindua miradi yenye thamani ya shilingi bil.1.6 wilayani Songwe
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250225-WA0009-2-2048x1203-1-950x558.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/waziri-kikwete-azindua-miradi-yenye.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/waziri-kikwete-azindua-miradi-yenye.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy