Waziri Mkenda Anena Mambo Mazito Akimkabidhi Ofisi Waziri Mpya Wa Kilimo
HomeHabari

Waziri Mkenda Anena Mambo Mazito Akimkabidhi Ofisi Waziri Mpya Wa Kilimo

Na Mathias Canal, Dodoma WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amekabidhi Ofisi kwa Waziri mpya wa Kilimo Hussein ...

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Septemba 4
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo September 3
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo


Na Mathias Canal, Dodoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amekabidhi Ofisi kwa Waziri mpya wa Kilimo Hussein Bashe huku alieleza kuwa amekabidhi kwa mtu anayejua vizuri.

Hayo ameyasema jijini Dodoma  tarehe 11 Januari 2022 wakati akikabidhi Ofisi kwa Waziri huyo Mara baada ya kuapishwa rasmi jana ambapo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru watumishi wa wizara hiyo kwa ushirikiano waliompa na kuwaaga.

“Nakabidhi ofisi kwa mtu anayejua wizara hii maana nilipokuja hapa nilimkuta mheshimiwa Hussein Bashe tumefanya kazi pamoja anaifahamu vizuri ofisi na mengi yaliyomo humu anayafahamu, nakutakia kila la heri kwenye utumishi wako,”.amesema Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati akikabidhi ofisi.

“Mimi na Bashe tumefanya kazi pamoja kwa ushirikiano mkubwa Kuna wakati mambo yalikuwa yakiwaka moto tunakutana haraka usiku ili kujadili na kutoka na msimamo mmoja,” amesema Profesa Mkenda

Amesema kilimo ni changamoto kubwa lakini kwa sasa kipo mikono salama na kuwataka waliobaki kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuondoa baadhi ya changamoto zilizobaki.

Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru watumishi wa wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati wa mchakamchaka wa utekelezaji majukumu yake.

Akizungumza Mara baada ya kukabidhiwa ofisi, Waziri Bashe amesema katika kipindi cha mwaka mmoja walichofanya kazi kwa pamoja misingi mizuri imejengwa ambayo yeye ataendelea kuifanyia kazi ili kuhakikisha kilimo kinasonga mbele.

“Tumefanya kazi mwaka mmoja ambao tumejenga misingi mizuri ambayo tutaendelea nayo sababu najua juhudi tulizofanya kufikia sehemu nzuri, tuna changamoto nyingi zinatukabili hivyo lazima tuzifanyie kazi, kwa kipindi cha mwaka mmoja nimepata ujuzi mkubwa kutoka kwako hivyo nakuahidi hakuna kilimo bila teknolojia wala Sayansi hivyo nitaendelea kukusumbua” Amekaririwa Mhe Bashe

Kadhalika, Waziri Bashe amemuimba Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Adolf Mkenda kutenge fedha kwa ajili ya kwenda kusomesha wataalamu wazuri wa kilimo nje ya nchi.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mkenda Anena Mambo Mazito Akimkabidhi Ofisi Waziri Mpya Wa Kilimo
Waziri Mkenda Anena Mambo Mazito Akimkabidhi Ofisi Waziri Mpya Wa Kilimo
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEg6QKyOBfWfNYxhz7baVslwGsM8xyIsyWAWAK29mjp01IlJX3FgyKnYxT-LIN-bu-CXRibqUnncuBKeUcu_A4k3b2SpzaM3jI-FTvuC1Wfw-etfUL3L3dkEnPRt4cga4BEij_nHGNFAIs6Vhxes-yPbO8OWffy0QCML61MVYNMfMLdEZgDVY7Vhz-Jchw=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEg6QKyOBfWfNYxhz7baVslwGsM8xyIsyWAWAK29mjp01IlJX3FgyKnYxT-LIN-bu-CXRibqUnncuBKeUcu_A4k3b2SpzaM3jI-FTvuC1Wfw-etfUL3L3dkEnPRt4cga4BEij_nHGNFAIs6Vhxes-yPbO8OWffy0QCML61MVYNMfMLdEZgDVY7Vhz-Jchw=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/waziri-mkenda-anena-mambo-mazito.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/waziri-mkenda-anena-mambo-mazito.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy