Tanzania, Marekani Zakubaliana Kuimarisha Ushirikiano
HomeHabari

Tanzania, Marekani Zakubaliana Kuimarisha Ushirikiano

Tanzania na Jimbo la Dallas la nchini Marekani  zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za utalii, michezo, uwekezaji   pamoja...

Majaliwa: Wakuu Wa Mikoa Msiwazuie Wananchi Kuingiza Mbolea Nchini
Waziri Kabudi Ataja Mafanikio Makubwa Sita Miaka 60 Ya Uhuru
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 13

Tanzania na Jimbo la Dallas la nchini Marekani  zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za utalii, michezo, uwekezaji   pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhifadhi wa maliasili pamoja na uendelezaji Utalii 
 
Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro  (Mb) pamoja na viongozi mbalimbali katika Jimbo la Dallas wakati walipofanya vikao vya ana kwa nyakati tofauti  kwa lengo la kujifunza namna wanavyoendesha shughuli za utalii pamoja kukuza ushirikiano baina ya pande zote mbili 
 
“Tumezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Jimbo la Dallas  pamoja na kuangalia namna tunavyoweza kuliteka soko la watalii katika Jimbo hilo, tumejadili mikakati ya kuanza na watalii ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu katika jimbo hilo lengo likiwa ni kupata soko la uhakika la  watalii wengi zaidi katika  siku za usoni ” Amesema Waziri Ndumbaro
 
Akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Jimbo la Dallas Liliana Rivera, Dkt. Ndumbaro amesema moja ya shabaha kubwa ni kuhakikisha kunaanzishwa  ndege ya moja kwa moja ya kutoka Tanzani kwenda Dallas ambapo amesema itaweza kusaidia  Watanzania ambao ni watalii kwenda Dallas na Watalii kutoka Dallas kutembelea Tanzania
 
” Tanzania imeshaanzxa mazungumzo na Uongozi wa Jimbo hilo ili kuhakikisha hilo linafanikiwa na hivi wiki lijalo Mkurugenzi wa Shrika la Ndege Tanzania (ATCL) atakuja Marekani kwa ajili ya kufanya mazungumzio hayo
 
Katika ziara hiyo pia,   Waziri Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mchezo wa Gofu nchini Marekani, Bruce Davidson ambapo Dkt.Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuinadi Tanzania kuwa  ipo  tayari kuwa  Mwenyeji wa mashindano makubwa  ya mchezo wa gofu yatayohusishwa Wachezaji mahiri wa mchezo huo
  
“ Mchezo wa gofu ni mchezo unaochezwa na watu wenye fedha nyingi hivyo kuwa wenyeji wa mashindano hayo tutapata fursa ya. kutangaza vivutio vya utalii kwa gharama nafuu kwa sababu wachezaji wakubwa pamoja na watu mashuhuri watakuja Tanzania , kupitia umaarufu wao vyombo vikubwa vya habari duniani vitaambatana nao kwa ajili ya kuripoti yatakayojiri” ameongeza Waziri Ndumbaro
 
Aidha, Katika mazungumzo hayo Dkt.Ndumbaro wamekubaliana kutangaza vivutio vya utalii kupitia mchezo huo kwa kutumia vyombo vya habari vya kimataifa vitakavyotumiwa katika kutangaza mchezom huo
 
Katika hatua nyingine, Waziri Ndumbaro  amekutana na kufanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mtendaji wa Dallas Safari Club, Corey Mason ambapo katika mazungumzo hayo wamezungumza maeneo ya kushirikiana ikiwemo kukuza utalii wa uwindaji na kutoa vifaa vya kukabiliana na  ujangili wa wanyamapori
 
Aidha, Katika mazungumzo hayo wamejadiliana  masuala ya Uwekezaji  ambapo Dkt.Ndumbaro amewaita Wawekezaji wa Marekani hususan Matajiri wa Jimbo la Dallas kuja kuwekeza Tanzani kwa kujenga mahoteli yenye hadhi ya nyota tano
 
Katika vikao hivyo vya Waziri Ndumbaro aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani  nchini Marerkani  Dkt. Elsie Kanza pamoja na Ujumbe wa kutoka Tanzania akwemo Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Brigedia Jenerali, Hamisi Semfuko, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi na Afisa Mwandamizi, Segoline Tarimo


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tanzania, Marekani Zakubaliana Kuimarisha Ushirikiano
Tanzania, Marekani Zakubaliana Kuimarisha Ushirikiano
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjtHnOQZiMA3nktxrUkS6Xp5D7m95OvymBJt3JaXMVVvUox3xOwmmTbP09pIzun3qjH-UpQBlPpF4IkX6r1UJ1uipM8H5QEGMaaT1UF62iTInXMoLQM1kdjF6D9HyXxLnJb3TwVkD9hhZUTeMjAsPQ5UlKIUC__Odx-Ly21iiWk0-y4fpvsHaMIMcwDuA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjtHnOQZiMA3nktxrUkS6Xp5D7m95OvymBJt3JaXMVVvUox3xOwmmTbP09pIzun3qjH-UpQBlPpF4IkX6r1UJ1uipM8H5QEGMaaT1UF62iTInXMoLQM1kdjF6D9HyXxLnJb3TwVkD9hhZUTeMjAsPQ5UlKIUC__Odx-Ly21iiWk0-y4fpvsHaMIMcwDuA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/tanzania-marekani-zakubaliana.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/tanzania-marekani-zakubaliana.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy