Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani katika vita dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria jana ulishambuli...
Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani katika vita dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria jana ulishambuliwa vikali, katika msururu wa mashambulizi ya karibuni zaidi ambayo Washington inasema yanafanywa na makundi yanayosaidiwa na Iran.
Hata hivyo hakukuripotiwa madhara yoyote. Mkuu wa muungano huo Jenerali John W. Brennan amekiri kwenye taarifa yake kwamba wanaendelea kushuhudia vitisho dhidi ya wanajeshi wao nchini Iraq na Syria kutoka kwa wanamgambo wanaosaidiwa na Iran.
Jana Jumatano maroketi matano yalililenga kambi ya vikosi vya anga vya muungano huo magharibi mwa Iraq.
Siku ya Jumanne vikosi hivyo vilifanikiwa kuzitungua ndege mbili zisizotumia rubani zilizokuwa zinaelekea kwenye kambi hiyo.
Mashambulizi hayo yanafanyika wakati Iran na washirika wake wa Mashariki ya Kati wakiadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa aliyekuwa kamanda wa majeshi la Iran Jenerali Qasem Soleimani.
Credit: MPEKUZI
Thanks for your time please share with your friends
COMMENTS