Balozi Mulamula: Misingi Ya Sera Ya Mambo Ya Nje Haijabadilika
HomeHabari

Balozi Mulamula: Misingi Ya Sera Ya Mambo Ya Nje Haijabadilika

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema kuwa Misingi ya Sera ya Mambo ya Nje haij...

Rais wa EALS Jaji Fauz kwenye Mashindano ya Wanasheria
Bandari ya Tanga sasa inashughulikia meli kubwa baada umya uwekezaji wa Bilioni 429
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo October 20, 2024


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema kuwa Misingi ya Sera ya Mambo ya Nje haijabadilika na iko imara, kusisitiza umoja na kutoshabiana kisiasa na upande wowote pamoja na kuwaunga mkono wale wote wanaokandamizwa.

Balozi Mulamula ameyasema hayo wakati alipokutana katika kikao kazi na watumishi wa Wizara Jijini Dodoma na kuwasihi watumishi kujenga mahusiano na kutekeleza kwa ufanisi Diplomasia ya Uchumi.

“Uchumi wa Tanzania unakuwa kutokana na juhudi zetu, na mtakumbuka kuwa Wizara ya Mambo ya Nje majukumu yake ni mtambuka kwani yanagusa kila sekta, na lengo la kikao hiki ilikuwa kukumbushana maagizo ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,”

“Nashukuru sana katika kukutana kwenye kikao na wafanyakazi binafsi nimehamasika na kuwa na ari mpya ya kuchapa kazi, na pia wafanyakazi wamehamasika mara baada ya kikao cha leo,”

Katika awamu ya Sita, Serikali imefungua balozi mbili mpya na Konseli mbili na naamini kutokana na msisitizo wa Mhe. Rais Samia wa kutekeleza Diplomasia ya uchumi kwa vitendo tutaendelea kufungua balozi nyingine zaidi kadri tutakapokuwa tunapata uwezo…….kile tulichonacho tukitumie vizuri kwani milango imefunguka.

Mazingira ni mazuri na ndiyo maana tunaendelea kuhamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kuja kuwekeza Tanzania.

Mwana Diplomasia namba moja Mhe. Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kutusaidia katika hili na hata juzi alipokutana na mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa aliweza kuwaeleza kuwa Tanzania ipo pamoja na kwamba tunaenda wote katika kufanikisha malengo ya watanzania yaweze kuboreka Zaidi.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Nassor Mbarouk (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Balozi Mulamula: Misingi Ya Sera Ya Mambo Ya Nje Haijabadilika
Balozi Mulamula: Misingi Ya Sera Ya Mambo Ya Nje Haijabadilika
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiBnI95jj9Q-1V7v0T_UkBTLTQ-qLQ7tHbc-2zSyAQSo4cXLlpjpWQT2zPOTtBBh_QbhUGtbyLvdUbc8o3XJuzePm1F8eZWxe0nId3qGM1SIz-6TMkTNYroi2-Gv3vcmKEcObOzCC9iuxp7EGgGqaOGQStTDGcsdwAn64OVUuOkJJ1L7VTvRHu0bCXrDA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiBnI95jj9Q-1V7v0T_UkBTLTQ-qLQ7tHbc-2zSyAQSo4cXLlpjpWQT2zPOTtBBh_QbhUGtbyLvdUbc8o3XJuzePm1F8eZWxe0nId3qGM1SIz-6TMkTNYroi2-Gv3vcmKEcObOzCC9iuxp7EGgGqaOGQStTDGcsdwAn64OVUuOkJJ1L7VTvRHu0bCXrDA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/balozi-mulamula-misingi-ya-sera-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/balozi-mulamula-misingi-ya-sera-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy