Rais Samia Amedhamiria Kulinda Na Kuimarisha Afya Za Watanzania-majaliwa
HomeHabari

Rais Samia Amedhamiria Kulinda Na Kuimarisha Afya Za Watanzania-majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kulinda na ...

Wamarekani waadhimisha siku ya Martin Luther King Jr.
Wananchi wamwapisha mwenyekiti wa mtaa
ACT wazichapa kavukavu Dar


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kulinda na kuimarisha afya za Watanzania hasa wakati huu tunapoelekea kutimiza dira ya kuutokomeza UKIMWI nchini ifikapo mwaka 2030.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Novemba 26, 2021) wakati akifungua Kongamano la Kisayansi la Kitaifa Kuhusu VVU na UKIMWI katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Modern Highland , jijini Mbeya. Kaulimbiu ya Kongamano hilo inasema “Zingatia Usawa, Tokomeza Ukimwi, Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko”.

Amesema kuwa kaulimbiu ya kongamano hilo inaakisi dhamira ya Serikali ya kulinda na kuimarisha afya za Watanzania hasa wakati huu tunapoelekea kutimiza Dira ya kuutokomeza UKIMWI nchini ifikapo mwaka 2030

“Hivyo basi, nitoe rai kwa jamii kutafakari upya nafasi waliyonayo na kupinga kwa nguvu zote masuala yote na tabia zinazochangia maambukizi mapya ikiwemo unyanyapaa, ukatili wa kijinsia, mila zinazochangia maambukizi, ngono katika umri mdogo, kuporomoka kwa maadili na tabia nyinginezo hatarishi.”

“Kaulimbiu hii, imekuja wakati muafaka ambapo kama Taifa tunahitaji kuihamasisha jamii na mtu mmoja mmoja kuzingatia usawa na kutoa mchango wake katika kufikia azma ya kutokomeza maambukizi mapya ya VVU hasa kwa vijana wetu ambao kwa mujibu wa Takwimu wanachangia kiwango kikubwa cha maambukizi mapya.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali kwa upande wake, itaendelea kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi kuchangia mfuko huu muhimu. Vilevile, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI pamoja na kutafuta vyanzo vya uhakika zaidi vya kutunisha mfuko huo.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kwa niaba ya Serikali kuwashukuru wadau wote wa maendeleo kwa kuendelea kufanya kazi na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya kudhibiti maambukizi mapya ya UKIMWI nchini. “Ninawahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nanyi katika kupambana na tatizo hili la UKIMWI.”

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ummy Nderiananga amesema kuwa wadau wote walioshiriki katika kongamano hilo watumie ujuzi na maarifa waliyopata katika kuboresha kazi zao “Pia taasisi zinazojihusisha na masuala ya VVU na UKIMWI waongeze nguvu kwa kundi la wenye ulemavu”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko amesema kongamano hilo ni fursa ya kuweza kutafakari walikotoka ili waweze kuendelea kutekeleza afua za VVU na UKIMWI.

Amesema kongamano hilo linawapa fursa nzuri ya kupata takwimu zinazowasaidia kuboresha utendaji kazi  ambapo ametoa mfano mwaka 2016/17 walifanya tafiti na kubaini wanaume wako nyuma katika suala zima la upimaji hivyo wanatakiwa wahamasishwe  ili nao wajitokeze kwa wingi kupima.

Naye, Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa PEPFAR Tanzania, Dkt. Hiltruda Temba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa dhamira ya dhati ya kutokomeza VVU na UKIMWI nchini pamoja na kuendelea kutoa kipaumbele katika huduma muhimu za kinga pamoja na utekelezaji mzuri wa afua za UKIMWI.

Pia, Dkt. Hiltruda amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa dhamira yake ya dhati ya kufikia malengo ya kuwa na asilimia 95 ya watu wanaoishi na VVU wanatambua hali zao za maambukizi, asilimia 95 ya watu wanaofahamu hali zao za maambukizi ya VVU wanapata tiba na asilimia 95 ya waliotumia dawa za ARV wamefanikiwa kupunguza kiasi cha maambukizi.

Dkt. Hiltruda amesema PEPFAR na wadau wengine wa maendeleo wanaahidi kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kufikia malengo yake ya kimkakati kama yalivyoainishwa kwenye mkakati wa nne wa Taifa wa VVU na UKIMWI.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia Amedhamiria Kulinda Na Kuimarisha Afya Za Watanzania-majaliwa
Rais Samia Amedhamiria Kulinda Na Kuimarisha Afya Za Watanzania-majaliwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjxnL7gmUZG8GVPewwRyJhZAdfkns7u2hW6C0SiQBJENx41SRd49O2qYqgmPxCdYi_fQ2kpu4My9anLhqSh6Y58qzuT9A5qmQIdFz6cQPSCww41jo8chH57RC01olE7-ABIx3RY_IC04ZgqyvaGolyQ1zeaB4VYJ0k23tIkR4YlTbWJSrt1rFjkAu7hrA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjxnL7gmUZG8GVPewwRyJhZAdfkns7u2hW6C0SiQBJENx41SRd49O2qYqgmPxCdYi_fQ2kpu4My9anLhqSh6Y58qzuT9A5qmQIdFz6cQPSCww41jo8chH57RC01olE7-ABIx3RY_IC04ZgqyvaGolyQ1zeaB4VYJ0k23tIkR4YlTbWJSrt1rFjkAu7hrA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/rais-samia-amedhamiria-kulinda-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/rais-samia-amedhamiria-kulinda-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy