KAZE ATAJA SABABU YA KUREJEA YANGA
HomeMichezo

KAZE ATAJA SABABU YA KUREJEA YANGA

 KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, amesema ametua kikosini hapo kuipa mataji, huku akisisitiza atashirikiana kikamilifu na Kocha Mkuu,...


 KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, amesema ametua kikosini hapo kuipa mataji, huku akisisitiza atashirikiana kikamilifu na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Kaze amewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu uliopita ambapo alifanikiwa kuipa Kombe la Mapinduzi kabla ya kusitishiwa mkataba wake na nafasi yake kuchukuliwa na Nabi.


Akizungumza na Spoti Xtra, Kaze alisema: “Ninafuraha kubwa kuona nimerudi ndani ya Yanga nikiwa kama kocha msaidizi, hivyo malengo ya timu ndio malengo yangu pia, nipo katika sehemu ya malengo ya timu ambayo ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa ligi kuu.


 “Hivyo nikishirikiana na Kocha Mkuu, Nabi naamini malengo yatafanikiwa japo hakuna safari ambayo haina mabonde na milima, tutapambana kuhakikisha changamoto zote tunazitatua ili tufanikiwe.”

Kaze alikuwa kwenye jukwaa wakati timu ya Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Simba na ilikuwa ni kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkapa, Septemba 25.

Tayari Ligi Kuu Bara imeanza kurindima ambapo leo kuna mechi tatu zinatarajiwa kuchezwa huku Yanga ikiwa na kibarua cha kufanya Septemba 29 dhidi ya Kagera Sugar.


 


Wakati Kaze akisema hivyo, Kocha wa Viungo wa Yanga, Helmi Gueldich, ametamba kuwa wana matumaini makubwa kikosi chao kitakuwa tishio zaidi msimu huu.


 


“Tumefanya usajili bora kwa ajili ya msimu huu, lakini pia tuna benchi bora la ufundi hasa baada ya kuwepo maboresho kwa kuongeza baadhi ya wakufunzi akiwemo Kaze na Zahera (Mwinyi), tuna matumaini ya kuwa na kikosi tishio zaidi,” alisema.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: KAZE ATAJA SABABU YA KUREJEA YANGA
KAZE ATAJA SABABU YA KUREJEA YANGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjo9bZwfq3QGYNsQ2yzw8H1cLENAWzuFhQDY4Rth6rL_EoBUIqPCfISzmkQWLToEJFg_zfPG7RH4mNEYcSe8xd49z10Icvdjz7wfpT5oX5IdQmoDr9gRJq5AcdXmPjHMfSClsRfgu8zXd5L/w640-h476/Kaze+na+Senzo.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjo9bZwfq3QGYNsQ2yzw8H1cLENAWzuFhQDY4Rth6rL_EoBUIqPCfISzmkQWLToEJFg_zfPG7RH4mNEYcSe8xd49z10Icvdjz7wfpT5oX5IdQmoDr9gRJq5AcdXmPjHMfSClsRfgu8zXd5L/s72-w640-c-h476/Kaze+na+Senzo.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/kaze-ataja-sababu-ya-kurejea-yanga.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/kaze-ataja-sababu-ya-kurejea-yanga.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy