Serikali Yakamilisha Mazungumzo Na Saudi Sudani Kuuza Unga Na Mtama Mweupe
HomeHabari

Serikali Yakamilisha Mazungumzo Na Saudi Sudani Kuuza Unga Na Mtama Mweupe

 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Iringa Serikali imekamilisha mazungumzo na kampuni ya ubia ya Saudi Sudani kwa ajili ya kuuza unga pam...

Tusiwe Sehemu ya Matumizi ya Nguvu wakati wa Uchaguzi.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 22, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 22, 2024

 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Iringa
Serikali imekamilisha mazungumzo na kampuni ya ubia ya Saudi Sudani kwa ajili ya kuuza unga pamoja na mtama mweupe.

Hiyo ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara nchini kwani wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo ambayo itakuwa sehemu ya muarobaini wa soko la nafaka kwa wakulima nchini.


Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 2 Agosti 2021 mjini Iringa mara baada ya kutembelea na kukagua kinu cha usagaji nafaka cha Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB).

Kuhusu kadhia ya uzalishaji duni wa mazao mbalimbali hususani nafaka Waziri Mkenda amesema kuwa serikali inaendela kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kuongeza tija kwenye mazao kadhalika kuongeza uzalishaji.

“Kuna uwezekano wa kuzalisha gunia 40 katika hekari moja hivyo ni lazima tuweke msisitizo kwenye kuongeza uzalishaji na tija” Amekaririwa Waziri Mkenda

Amesema kuwa pamoja na kuongeza tija na uzalishaji lakini ili kufikia hatua kubwa katika uzalishaji na tija hivyo ni lazima kuimarisha sekta ya mbegu na kuwa na upatikanaji wa mbegu bora nchini.

Kuhusu bei ya mahindi, Prof Mkenda amesema kuwa bei ya mahindi iliporomoka hivi karibuni ambapo aliagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB)  kuingia sokoni ili kununua nafaka hususani mahindi jambo ambalo limeanza kuimarisha bei ya mahindi.

Katika ziara hiyo ya Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda kwenye mikoa ya Nyanda za juu kusini imejikita katika kugagua hali ya upatikanaji wa mbolea, ununuzi wa mahindi pamoja na kukagua skimu za umwagiliaji.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Yakamilisha Mazungumzo Na Saudi Sudani Kuuza Unga Na Mtama Mweupe
Serikali Yakamilisha Mazungumzo Na Saudi Sudani Kuuza Unga Na Mtama Mweupe
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4Vq6_NyHlE1go7NzfS-RgTVIDeDGdlfm7gMIo861-egi7kKjcORbq1Bw22kMisPVxPGauqV-bRHf22ZcFRzxq7TrNWi6puf78_8EtHMVzCLzXsDE_auSZzP6yD8KKHrRG4hewqMn9m9V_/s0/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4Vq6_NyHlE1go7NzfS-RgTVIDeDGdlfm7gMIo861-egi7kKjcORbq1Bw22kMisPVxPGauqV-bRHf22ZcFRzxq7TrNWi6puf78_8EtHMVzCLzXsDE_auSZzP6yD8KKHrRG4hewqMn9m9V_/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/serikali-yakamilisha-mazungumzo-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/serikali-yakamilisha-mazungumzo-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy