Dr. Gwajima: Tulihimiza Matumizi Ya Tiba Asili Kwa Sababu Hapakuwa Na Njia Nyingine Ya Kupambana Dhidi Ya Corona
HomeHabari

Dr. Gwajima: Tulihimiza Matumizi Ya Tiba Asili Kwa Sababu Hapakuwa Na Njia Nyingine Ya Kupambana Dhidi Ya Corona

 Na WAMJW- Nairobi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameweka wazi kuwa Serikali ya Tanzani...

Wananchi Lupembe wapunguziwa adha ya kukodi usafiri kwa ajili ya wagonjwa 
“Wanawake wajasiriamali wapewa mafunzo maalum,Aweso atoa Mil 10 kuwawezesha”
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 1, 2024

 Na WAMJW- Nairobi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameweka wazi kuwa Serikali ya Tanzania ilihimiza matumizi ya tiba asili wakati wa mlipuko wa wimbi la kwanza la Corona kwa kuwa zilionesha kuwasaidia watu wengi kwenye kipindi hicho ambapo Dunia haikuwa na njia mbadala yoyote ya kupambana dhidi ya Corona ukilinganisha na uwepo wa chanjo katika kipindi hiki.

Dkt. Gwajima amesema hayo wakati akiongea na Waandishi wa habari wa nchini Kenya ambapo wamefanya mkutano wa pamoja wa kujadili changamoto zinazowakabili nchi hizo mbili ikiwemo ya UVIKO-19 kwa upande wa mipakani.

“Ugonjwa huu uliingia Wuhan nchini China Disemba 2019, wakati Dunia ilikuwa haielewi ifanye nini, Dunia nzima ilikuwa haina chanjo, haina formula ya dawa, haielewi ifanye nini kwa mfano; wakati huo nyoka ameshaingia ndani na wewe ndio mama na Watoto wamekuzunguka na nyoka yupo mlangoni, inatakiwa unapigana kwa mwiko kwa kummwagia uji au kwa chochote na ndivyo ilivyokuwa ” alisema

Aliendelea kusema kuwa, Tiba asili Kwa upande wa Tanzania lipo Baraza la kitaalamu kisheria ambayo imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kiasi kikubwa zimeonesha kusaidia watu wenye matatizo ya kifua kwa kuona umuhimu katika mapambano hayo ilikuwa ni muhimu kutumia tiba hizo ili kunusuru maisha ya Watanzania.

Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema kuwa, Tiba asili zilikuwepo toka zamani kabla ya dawa nyingine hazijaja, na zilisaidia kutibu magonjwa mengi, hata katika vita dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona kwenye wimbi la kwanza tiba asili ilionesha mafanikio makubwa sana.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema kuwa, licha ya kutumia tiba asili katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona, Serikali ilihimiza wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga nyingine ikiwemo kufanya mazoezi, kula chakula bora (lishe bora), kuvaa Barakoa, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na kuepuka misongamano isiyo yalazima.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dr. Gwajima: Tulihimiza Matumizi Ya Tiba Asili Kwa Sababu Hapakuwa Na Njia Nyingine Ya Kupambana Dhidi Ya Corona
Dr. Gwajima: Tulihimiza Matumizi Ya Tiba Asili Kwa Sababu Hapakuwa Na Njia Nyingine Ya Kupambana Dhidi Ya Corona
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgrpMbQZq3Up4qEkWK8SlQ45hrGn7_Z9r3qQ3S1I8GOSvR4oFR6_2I85cXeNGGEqXRjr5wB3igQEsFFi4Md0XlR4VBv-G8F5wjeqagVXYW1asolbjf3ZO2qLEexLiCQ5X8WZvUxv3hIZGDa/s0/1.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgrpMbQZq3Up4qEkWK8SlQ45hrGn7_Z9r3qQ3S1I8GOSvR4oFR6_2I85cXeNGGEqXRjr5wB3igQEsFFi4Md0XlR4VBv-G8F5wjeqagVXYW1asolbjf3ZO2qLEexLiCQ5X8WZvUxv3hIZGDa/s72-c/1.png
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/dr-gwajima-tulihimiza-matumizi-ya-tiba.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/dr-gwajima-tulihimiza-matumizi-ya-tiba.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy