KOCHA ATOA MASHARTI ISHU YA USAJILI, YANGA KUSAJILI WATANO
HomeMichezo

KOCHA ATOA MASHARTI ISHU YA USAJILI, YANGA KUSAJILI WATANO

  K OCHA Mkuu wa kikosi cha  Yanga, Nasreddine Nabi  ameuambia uongozi wa timu  hiyo kuwa, hataki kuona wakirudia  makosa waliyofanya misi...

EXCLUSIVE:MEDDIE KAGERE AFUNGUKIA ISHU YAKE KUITWA MZEE
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
SIMBA MWENDO WA DOZI TU, YAIVUTIA KASI YANGA

 KOCHA Mkuu wa kikosi cha Yanga, Nasreddine Nabi ameuambia uongozi wa timu hiyo kuwa, hataki kuona wakirudia makosa waliyofanya misimu miwili iliyopita kwenye dirisha la usajili kwa kusajili wa nyota wengi wapya na kuacha idadi kubwa ya wachezaji.

 

Kwa misimu miwili iliyopita, Yanga imekuwa na kawaida ya kusajili nyota wengi wapya, huku pia ikitangaza kuachana na kundi kubwa la wachezaji ambapo kwa msimu uliopita pekee waliachana na wachezaji 14.

 

Yanga ambao wanakamatia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, wamedhamiria kuhakikisha wanarudisha utawala wao katika michuano mbalimbali watakayoshiriki msimu ujao, utawala ambao kwa sasa unaonekana kuchukuliwa na wapinzani wao wa jadi, Simba.


Akizungumzia mipango yao ya usajili Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema:

 

“Kocha mkuu wa kikosi chetu, Nasreddine Nabi amesema anafurahishwa na ubora wa kikosi tulichonacho, na kuhusiana na maboresho kupitia usajili wa wachezaji wapya, kocha ameutaka uongozi kufanya usajili wa wachezaji watano au sita kwa ajili ya kuongeza nguvu.


"Kocha Nabi hataki kuona tunaondoa wachezaji wengi kwa mara moja kama ambavyo ilitokea kwa misimu miwili iliyopita, hivyo tunatarajia kuachana na baadhi ya wachezaji wakiwemo wanaomaliza mikataba yao, ili kutoa nafasi ya nyota wapya ambao watatangazwa,".

 

Akizungumza na Championi Jumamosi,Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Injinia Hersi Said kuhusu mipango ya usajili alisema: “Sisi kama GSM tumetenga dau kubwa la usajili wa nyota wapya, tunataka kutengeneza timu bora si tu kwa mashindano ya ndani, bali timu itakayofanya vizuri na kuweka rekodi kimataifa.”


Miongoni mwa wachezaji ambao wamesajili hivi karibuni na Yanga na wanatajwa kuwa kwenye mpango wa kuachwa mazima ni pamoja na Lamine Moro, Michael Sapong ambao hawa ni raia wa Ghana.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: KOCHA ATOA MASHARTI ISHU YA USAJILI, YANGA KUSAJILI WATANO
KOCHA ATOA MASHARTI ISHU YA USAJILI, YANGA KUSAJILI WATANO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkQMKqQP57N8E-rUP2KGRBLBYVhF5PFtMaa1EmUHSoQf_j9cBO1Zy8PdRSYRU4JW3xuqGRcFeoQ2_OdGiOFSPTd11r4CvdFEq0mO_JjGkbPRY7QLPlyXC1jOE8clGtdVz2Ue9S2Oy7IbgP/w622-h640/finally_sarpong19-119691057_325553191989069_7017791267500802946_n.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkQMKqQP57N8E-rUP2KGRBLBYVhF5PFtMaa1EmUHSoQf_j9cBO1Zy8PdRSYRU4JW3xuqGRcFeoQ2_OdGiOFSPTd11r4CvdFEq0mO_JjGkbPRY7QLPlyXC1jOE8clGtdVz2Ue9S2Oy7IbgP/s72-w622-c-h640/finally_sarpong19-119691057_325553191989069_7017791267500802946_n.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/kocha-atoa-masharti-ishu-ya-usajili.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/kocha-atoa-masharti-ishu-ya-usajili.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy