Dkt. Ndugulile Aitaka TCRA Kuelimisha Umma Na Kuboresha Mifumo Ya Malalamiko
HomeHabari

Dkt. Ndugulile Aitaka TCRA Kuelimisha Umma Na Kuboresha Mifumo Ya Malalamiko

 Na Faraja Mpina, WMTH, Dodoma Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Ta...

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 13, 2024
Waziri Biteko aagiza kuchukuliwa hatua za kisheria Mtanzania anedaiwa kukutwa na shehena kubwa ya nyaya za Tanesco
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 12, 2024


 Na Faraja Mpina, WMTH, Dodoma
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) kuboresha vitengo vyao vya mawasiliano ili kuongeza kasi ya kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano kwa kuzingatia haki na wajibu pamoja na matumizi sahihi ya simu janja na mtandao.

Dkt. Ndugulile amezungumza hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya kikao chake cha kazi cha Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo cha kujadili na kufanya mapitio ya taarifa za mapato na matumizi za taasisi hizo kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/2021 Kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Aidha Dkt. Ndugulile ameziagiza taasisi hizo kuboresha mifumo ya wananchi kutolea malalamiko yanayohusu huduma za mawasiliano na kushughulikia malalamiko hayo kwa wakati na taarifa ya malalamiko hayo itakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vya kila robo mwaka baina ya Wizara hiyo na taasisi zake.

Ameongeza kuwa elimu kwa umma ikitolewa kwa kiwango kinachojitosheleza kitapunguza baadhi ya malalamiko ya wananchi kwa mfano malalamiko ya vifurushi vya data kuisha haraka ambapo kwa namna moja ama nyingine inasababishwa na settings za simu janja kuruhusu programu zake kujiboresha zenyewe (automatic Updating).

“Kuna mambo ambayo ni muhimu wananchi kuyafahamu kwa mfano matumizi makubwa ya data yanayosababishwa na settings za simu janja ambazo zinaruhusu baadhi ya programu kujiboresha zenyewe nazo zinachangia vifurushi vya data kuisha haraka”, alizungumza Dkt. Ndugulile

Aliongeza kuwa Serikali inatengeneza mazingira wezeshi ya kuhakikisha mawasiliano yanafika kwa wananchi wote lakini kumekuwa na changamoto ya baadhi ya watu kutokuwa na matumizi sahihi ya huduma hii, hivyo wananchi wanahitaji kuelemishwa ili kuhakikisha wanajua wajibu wao na haki zao na kuwa na matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Akizungumzia kikao cha Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo cha mapato na matumizi Dkt. Ndugulile amesema kuwa lengo ni kusimamia nidhamu na matumizi ya fedha za taasisi hizo badala ya kusubiri mpaka  mwisho wa mwaka CAG aje kuhoji.

“Sisi kama Wizara tunajipanga kuhakikisha fedha zinazopatikana zinaelekezwa katika kutekeleza majukumu ya msingi ya Wizara na taasisi zake ikiwa ni pamoja na kwenda kutekeleza miradi ya maendeleo.

Dkt. Ndugulile amezielekeza taasisi zilizo chini ya Wizara yake kutolea ufafanuzi maeneo ambayo yaliguswa katika taarifa ya CAG na kama kuna hoja zozote ziliyojitokeza zijibiwe kikamilifu na kuwasilishwa ndani ya wiki ijayo na taasisi ambazo hazikuwasilisha hesabu zao kwa CAG watoe maelezo kwa nini hawakuziwasilisha kwa mujibu wa taratibu za Serikali

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Kundo Mathew amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kutambua kuwa Wizara inayowasimamia ipo makini kuhakikisha taasisi hizo zinatimiza wajibu wake wa kuhudumia wananchi na yeye kama msaidizi wa Waziri mwenye dhamana atashirikiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Naibu wake kuhakikisha kuwa Wizara na taasisi zake zinafanya kazi zenye ubora na kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuandaa taarifa zinazojitosheleza bila kusubiri maelekezo.

 Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula, Naibu wake Dkt Jim Yonazi, Wakuu wa taasisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Tume ya Taifa ya Tehama (ICTC), Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC), Menejimenti ya Wizara pamoja na baadhi ya watendaji wa taasisi zake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt. Ndugulile Aitaka TCRA Kuelimisha Umma Na Kuboresha Mifumo Ya Malalamiko
Dkt. Ndugulile Aitaka TCRA Kuelimisha Umma Na Kuboresha Mifumo Ya Malalamiko
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjm154rbBLDVxB2xKj12X7eBk623dOAHiImRSzQM66sZ3I3XK2y7Wa0QLikQ7-3RfMebdroOpxQGwdq8k8mE9cmgm5jTW35WhjlgSA-Y6t2TQJPY2P_rnsr72bmLs3p_kd0JWfp2n1i6pEE/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjm154rbBLDVxB2xKj12X7eBk623dOAHiImRSzQM66sZ3I3XK2y7Wa0QLikQ7-3RfMebdroOpxQGwdq8k8mE9cmgm5jTW35WhjlgSA-Y6t2TQJPY2P_rnsr72bmLs3p_kd0JWfp2n1i6pEE/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/dkt-ndugulile-aitaka-tcra-kuelimisha.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/dkt-ndugulile-aitaka-tcra-kuelimisha.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy