Kamati Za Uchunguzi Zinazoundwa Na Mamlaka Za Ajira Na Mamlaka Za Nidhamu Zinapaswa Kuthibitisha Tuhuma Zinazowakabili Watumishi Wa Umma
HomeHabari

Kamati Za Uchunguzi Zinazoundwa Na Mamlaka Za Ajira Na Mamlaka Za Nidhamu Zinapaswa Kuthibitisha Tuhuma Zinazowakabili Watumishi Wa Umma

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mstaafu) Mheshimiwa Dkt. Steven J. Bwana amezitaka Kamati za Uchunguzi zinazoundwa kuchungu...

Taarifa Kwa Umma: Tuhuma Za Rushwa Ya Ngono Zinazomkabili Mtumishi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Ndugu Petro Bazil Mswahili
Waziri Mhagama Akemea Utoro Wa Dawa Kwa wanaoishi na Virusi vya UKIMWI
Maambukizi ya kichocho yazidi kupanda wilaya ya Itilima.


Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mstaafu) Mheshimiwa Dkt. Steven J. Bwana amezitaka Kamati za Uchunguzi zinazoundwa kuchunguza tuhuma wanazokabiliwa nazo watumishi wa umma kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kuziwezesha  Mamlaka za Nidhamu kutoa uamuzi wa  haki.

Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Bwana amesema haya wakati wa Mkutano wa Nne kwa mwaka 2020/2021 wa Tume ya Utumishi wa Umma  unaoendelea kufanyika Jijini Dar es Salaam.

 “Kamati za Uchunguzi zinazoundwa na Mamlaka za Nidhamu zina wajibu wa kufanya kazi yake kama inavyoelekezwa katika Hadidu za Rejea wanazopatiwa.  Kamati hizi zinatakiwa kufanya kazi yake kwa weledi mkubwa ili kuthibitisha au kutothibitisha tuhuma, makosa wanayotuhumiwa nayo watumishi ili kuondoa utata. Baadhi ya Kamati hizi zinashindwa kufanya kazi yake ipasavyo na kusababisha baadhi ya Mamlaka za Nidhamu kujielekeza vibaya katika kuhitimisha mashauri ya nidhamu” alisema Jaji (Mstaafu) Dkt. Bwana.

Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Bwana alisema katika kupitia rufaa na malalamiko yanayowasilishwa mbele ya Tume baadhi ya mashauri yamekuwa yakiamuliwa na Tume kuwa yaanzishwe upya na Mamlaka za Nidhamu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo, hii ni kwa sababu Kamati za Uchunguzi zimeshindwa kutoa uthibitisho, kuondoa utata kama kweli makosa anayotuhumiwa kutenda  mtumishi yamethibitika.

“Ni muhimu sana kwa Kamati za Uchunguzi kuzitumia Hadidu za Rejea wanazopewa kuwawezesha kutoa ripoti nzuri. Wanapaswa kusema katika ripoti zao  yale waliyoyaona na kuyabaini  kwa ukweli. Watambue kazi yao kubwa ni kuthibitisha au kutothibitisha tuhuma ili haki iweze kutendeka” alisisitiza Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Bwana.

Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Immaculata Ngwale alisema Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu zinapaswa kuwa makini wakati wa kushughulikia masuala ya Nidhamu kwa Watumishi walio chini yao.

“Hadidu za Rejea wanazopatiwa Kamati ya Uchunguzi zinapaswa kulenga katika kupata matokeo, kuchunguza tuhuma, kuthibitisha au kutothibitisha makosa ili haki itendeke. Pale Mamlaka za Nidhamu zinapoona Hadidu za Rejea ilizotoa zina upungufu ni muhimu sana zirejee Taratibu na Miongozo iliyopo na lengo liwe ni kuhitimisha mashauri haya kwa haki” alisema Mheshimiwa Ngwale.

Mkutano wa Tume utaendelea kesho kwa mujibu wa ratiba na  utahitimishwa tarehe 02 Julai, 2021.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Kamati Za Uchunguzi Zinazoundwa Na Mamlaka Za Ajira Na Mamlaka Za Nidhamu Zinapaswa Kuthibitisha Tuhuma Zinazowakabili Watumishi Wa Umma
Kamati Za Uchunguzi Zinazoundwa Na Mamlaka Za Ajira Na Mamlaka Za Nidhamu Zinapaswa Kuthibitisha Tuhuma Zinazowakabili Watumishi Wa Umma
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQ6yPP7CNXsm_SNlT9x2VfkP4fyB9EdScLGrAunera3PujbzsGnri7stkxi8BnEXCqb87RANr9od3S6l4VxRzZbvQSj3fvFLiOj4Ey-y8gkh0_Rqu-L4Nf-L1TT8Y042FkSR-Q26MVXuUf/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQ6yPP7CNXsm_SNlT9x2VfkP4fyB9EdScLGrAunera3PujbzsGnri7stkxi8BnEXCqb87RANr9od3S6l4VxRzZbvQSj3fvFLiOj4Ey-y8gkh0_Rqu-L4Nf-L1TT8Y042FkSR-Q26MVXuUf/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/kamati-za-uchunguzi-zinazoundwa-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/kamati-za-uchunguzi-zinazoundwa-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy