Nchini Kenya, karibia wanafunzi 17 wa Shule ya msingi ya kibinafasi ya Hillside Endarasha Academy iliyopo katika Kaunti ya Nyeri, katika mko...
Nchini Kenya, karibia wanafunzi 17 wa Shule ya msingi ya kibinafasi ya Hillside Endarasha Academy iliyopo katika Kaunti ya Nyeri, katika mkoa wa kati, wamethibitishwa kupoteza maisha, baada ya kuteketea kwa moto wakiwa bwenini.
Msemaji wa polisi Resila Onyango amethibitisha tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo na kuongeza kuwa wanafunzi wengine 14 wamejeruhiwa vibaya, na wamekimbizwa hospitalini.
Inaelezwa kwamba moto huo ulianza usiku wa kuamkia leo wakati wanafunzi hao wakiwa wamelala kwenye bweni lao.
“Kuna wanafunzi 17 ambao wamethibitishwa kufariki wakati wengine wakiwa wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya.” amesema msemaji wa polisi Resila Onyango.
Licha ya kuthibitisha mkasa huo, maofisa wa polisi hawajatoa maelezo kuhusu umri wa waathiriwa wa mkasa huo.
Aidha msemaji huyo wa polisi ameeleza kwamba miili ambayo imeondolewa kwenye eneo la mkasa imechomeka kiasi cha kutotambulika.
The post Karibia wanafunzi 17 wameteketea kwa moto wakiwa bwenini first appeared on Millard Ayo.
from Millard Ayo https://ift.tt/ZKWhnI8
COMMENTS