Maambukizi ya kichocho yazidi kupanda wilaya ya Itilima.
HomeHabari

Maambukizi ya kichocho yazidi kupanda wilaya ya Itilima.

 Samirah Yusuph, Itilima. Maambukizi ya minyoo tumbo inayosababisha ugonjwa wa kichocho wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu yamezidi kupanda...

Uwekezaji Kwenye Dagaa Ni Muhimu Kiafya Na Kiuchumi
Waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2022 ....Tazama Hapa
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 25


 Samirah Yusuph,
Itilima. Maambukizi ya minyoo tumbo inayosababisha ugonjwa wa kichocho wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu yamezidi kupanda kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 57 kwa mwaka huu 2021.

Taarifa hiyo imetolewa na mganga mkuu wa wilaya hiyo Anord Musiba alipokuwa katika uzinduzi wa zoezi la unyweshaji dawa za minyoo kwa watu wazima lililofanyika jana Octoba 27,2021 katika kata ya Budalabujiga wilayani hapo.

Musiba alisema kuwa wilaya hiyo imekuwa na idadi kubwa ya maambukizi katika kata 12 ambapo baadhi ya kata zinakiwango kikubwa cha maambukizi hadi kufikia zaidi ya asilimia 60.

"Dawa zinazotolewa ni kinga pia ni tiba ikiwa wananchi watabadili mtindo wa maisha kwa kufuata matumizi sahihi ya choo, kunawa mikono, kutumia maji safi na salama pamoja na kuepuka kuoga katika madimbwi".

Akielezea mkakati wa kupambana na maambukizi hayo mkuu wa wilaya ya Itilima, Faiza Salim alisema hatua ya unyweshaji dawa ni mwanzo wananchi wanawajibu wa kuhakikisha wanazingatia usafi katika maeneo yao pamoja kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo ili kuzuia maambukizi.

Amesema bila kuzuia maambukizi katika ngazi ya chini zoezi la unyweshaji wa dawa litakuwa halina mafanikio kwa sababu bado matumizi ya choo ni madogo wananchi bado wanajisaidia vichakani.

"Hivyo watendaji wa vijiji lazima wahakikishe katika maeneo yao wananchi wanatumia vyoo na kila kaya inakuwa na choo ili kukabiliana na maambukizi haya"

Baadhi ya wananchi wa kata ya Budalabujiga walieleza kuwa zoezi hili limekuwa ni hamasa kwa wananchi ambao awali walikuwa na imani potofu ya kudhani kuwa dawa zinazotolewa zinamadhara kwa binadamu.

"Wengi hawatumii vyoo kwa sababu walizoea  kwenda vichakani kwa sasa tunaendelea kuhamasisha wananchi wajenge vyoo na kuvitumia ili kupambana na kichocho" Alisema Masho Lukuba mwenyekiti wa kijiji cha Budalabujiga.

Meneja wa mradi wa kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka shirika lisilo la kiserikali world vision, Irene Abusheikh alisema wamejipanga kupunguza na kutokomeza kichocho.

"Zoezi litafanyika kwa watoto kuanzia miaka 5 hadi wazee lengo ni kuboresha na kudumisha  ustawi wa familia na jamii kwa ujumla"

Zoezi la utoaji wa dawa za kichocho litafikia wananchi 136,000 wa wilaya ya Itilima katika kata 12 ambazo zimepewa kipaumbele kutokana na maambukizi ya kichocho kuwa katika kiwango cha juu.

Mwisho.





Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Maambukizi ya kichocho yazidi kupanda wilaya ya Itilima.
Maambukizi ya kichocho yazidi kupanda wilaya ya Itilima.
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjIPxCAefzl1LHcxEW6PqMD7yyN3W0ffOAQixVx3wn9Su3nw1jRGmKW3hOtj3QsfEmBSsArexWxRKn2QWnpf-ofB-6mJYY61Gb8Lkuwy-GwUHt_bLAp821u_TlB6gmqDp9ZipIB39XorQtWo6E74wumB1l11sqMpKKNhSUSp-Cxs_eQQ3wvlhEYyy_m2g=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjIPxCAefzl1LHcxEW6PqMD7yyN3W0ffOAQixVx3wn9Su3nw1jRGmKW3hOtj3QsfEmBSsArexWxRKn2QWnpf-ofB-6mJYY61Gb8Lkuwy-GwUHt_bLAp821u_TlB6gmqDp9ZipIB39XorQtWo6E74wumB1l11sqMpKKNhSUSp-Cxs_eQQ3wvlhEYyy_m2g=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/maambukizi-ya-kichocho-yazidi-kupanda.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/maambukizi-ya-kichocho-yazidi-kupanda.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy