Dkt. Mollel Atoa Onyo Kwa Watumishi Wanaotoka Kazini Muda Wa Kazi Na Kwenda Kufanya Kazi Binafsi
HomeHabari

Dkt. Mollel Atoa Onyo Kwa Watumishi Wanaotoka Kazini Muda Wa Kazi Na Kwenda Kufanya Kazi Binafsi

  Na WAMJW, DODOMA Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa onyo kwa watumishi wa sekta ya afya wanaotoka kazini muda wa kazi na ...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo October 11, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo October 10, 2024
TARI NA TOSCI watoa mafunzo kwa wakulima wazalishaji mbegu za Mtama, Kanda ya Ziwa na Magharibi


 Na WAMJW, DODOMA
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa onyo kwa watumishi wa sekta ya afya wanaotoka kazini muda wa kazi na kwenda kufanya kazi binafsi.

Dkt. Mollel amesema hayo jana mara baada ya kufanya kikao kazi na mameneja wa Mikoa toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini NHIF leo Jijini Dodoma.

“Waziri wa Afya aliunda timu na ikaonyesha jinsi ambavyo kuna ubadhirifu mkubwa kwenye eneo la dawa, kuna madaktari hawakai wakati wa kazi, dawa zinaibiwa na kukosesha huduma kwa wananchi na kuikosesha Serikali mapato” amesema Dkt. Mollel.

Dkt. Mollel ameonyesha kushangazwa na viongozi ndani ya maeneo husika kushindwa kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi wenye tabia hizo huku akisisitiza watumishi wenye tabia hizo kujirekebisha kabla ya yeye kuanza kuchukua hatua za kisheria.

“Kila mtu acheze kwenye namba yake sasa, usipocheza kwenye namba yako imekula kwako, usifikiri usipocheza kwenye namba yako itamhusu yule aliyefanya kosa, itakuhusu na wewe ambaye ulitakiwa uone” Amesema kwa lugha ya mafumbo akimaanisha kila mtumishi atimize wajibu wake kwenye nafasi yake pamoja na viongozi kuchukua hatua mapema.

Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa amepanga kukutana wa wasajili wa vituo binafsi kuzungumza nao jinsi ya kuweka mipango endelevu ya kutumia wataalam waliopo katika sekta ya afya.

Dkt. Mollel ametoa onyo pia kwa wamiliki wa vituo binafsi vya kutolea huduma za afya nchini kuhakikisha wanafuata taratibu zote walizopewa kwenye usajili wa vituo hivyo na kuacha kutumia watumishi wa umma kinyume na taratibu za muda wa kazi.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt. Mollel Atoa Onyo Kwa Watumishi Wanaotoka Kazini Muda Wa Kazi Na Kwenda Kufanya Kazi Binafsi
Dkt. Mollel Atoa Onyo Kwa Watumishi Wanaotoka Kazini Muda Wa Kazi Na Kwenda Kufanya Kazi Binafsi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzrWo46vDfxaZP0TZiqnARDZUFuxEfx-5yRW59Dq2GnSIpxdQvLjMUvx-SIYW3WLiGoAaPmZnPRX09s2d6DxQ1ct7jcgDukdRP9DqkHfuZdRfmqYaSaKY1AkALRD5H_AuxFCfFN0Tzfgko/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzrWo46vDfxaZP0TZiqnARDZUFuxEfx-5yRW59Dq2GnSIpxdQvLjMUvx-SIYW3WLiGoAaPmZnPRX09s2d6DxQ1ct7jcgDukdRP9DqkHfuZdRfmqYaSaKY1AkALRD5H_AuxFCfFN0Tzfgko/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/dkt-mollel-atoa-onyo-kwa-watumishi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/dkt-mollel-atoa-onyo-kwa-watumishi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy