Dkt. Godwin Mollell: Wataalam Chukueni Vipimo, Msiangalie Pekee Kwenye Tatizo La Upumuaji Ili Kumtambua Mgonjwa Wa Corona
HomeHabari

Dkt. Godwin Mollell: Wataalam Chukueni Vipimo, Msiangalie Pekee Kwenye Tatizo La Upumuaji Ili Kumtambua Mgonjwa Wa Corona

Na Englibert Kayombo, WAMJW – Arusha Wataalam wa Afya nchi wametakiwa kuchukua vipimo kwa washukiwa wa ugonjwa wa corona na sii kuangal...

Boda boda wilaya ya handeni wafanya maandano na kufanya usafi kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluh Hassan
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 25, 2024
UWT wamshika mkono kijana mwenye ulemavu wilayani Makete


Na Englibert Kayombo, WAMJW – Arusha

Wataalam wa Afya nchi wametakiwa kuchukua vipimo kwa washukiwa wa ugonjwa wa corona na sii kuangalia kwenye tatizo la upumuaji pekee.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel alipokuwa ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru kujionea hali ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona.

“Tunakubali kuwa ugonjwa upo lakini tunawataka wataalam wetu wa afya kufanya vipimo zaidi na kujiridhisha kuwa ni ugonjwa wa corona au ni matatizo tuu ya kawaida ya upumuaji” amesema Dkt. Mollel

Ametolea mfano wa Hospitali ya Mount Meru ambayo hadi leo ilikuwa na washukiwa 44 wa ugonjwa corona huku wagonjwa waliopimwa na kuthibitishwa kuwa na ugonjwa wa corona walikuwa ni 4.

Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa hali ya ugonjwa huo inasimamiwa vizuri na wataalam wa afya nchini huku akiwatoa hofu wananchi kuwa idadi ya wagonjwa hao waliopo nchini kuwa sii kubwa.

“Licha ya kuwa na idadi ndogo ya wagonjwa wa corona haimaanishi tusiendelee kuchukua hatua hapana, sasa wimbi la tatu la ugonjwa wa corona hapa nchini, tuendelee kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na wataalam wetu, tuzingatie kunawa mikono mara kwa mara, kuvaa barakoa pamoja na kuepuka mikusanyiko” amesisitiza Dkt. Mollel

“Tuendelee kufanya yote kwa namna ya kujikinga toka kwenye wimbi la kwanza, la pili na sasa tuko kwenye wimbi la tatu, zile taratibu zote ambazo zimetufanya sisi tupite salama kipindi kile nazo tuendelee kufanya zikiwemo kula matunda pamoja na kutumia tiba asili katika kujikinga dhidi ya ugonjwa huu” amefafanua zaidi Dkt. Godwin Mollel

Dkt. Mollel amesema kuwa katika wimbi hili la tatu kirusi cha ugonjwa wa corona kimekuwa kikali na tofauti kama ilivyokuwa katika wimbi la kwanza na pili kupelekea Wizara kuja na mkakati mpya wa kutoa elimu zaidi juu ugonjwa huo pamoja na kupita kwenye hospitali kujionea hali halisi ya ugonjwa wa corona kwenye vituo hivyo vya kutolea huduma za afya nchini.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bi. Vones Uisso amemshukuru Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kutembelea Mkoa wa Arusha hususani Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Bi. Uisso amesema kuwa Uongozi wa Mkoa umejipanga kuendelea kutoa elimu kwa umma na kuwatahadharisha wananchi kufuata maelekezo yote yanayotolewa na viongozi pamoja na wataalam wa afya.

Amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imepanga kufanya kikao cha pamoja na viongozi wote kuanzia ngazi ya kijiji mpaka mkoani kuweka mikakati endelevu ya uhamasishaji wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa wa corona.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt. Godwin Mollell: Wataalam Chukueni Vipimo, Msiangalie Pekee Kwenye Tatizo La Upumuaji Ili Kumtambua Mgonjwa Wa Corona
Dkt. Godwin Mollell: Wataalam Chukueni Vipimo, Msiangalie Pekee Kwenye Tatizo La Upumuaji Ili Kumtambua Mgonjwa Wa Corona
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3o793dV8VX3E7JTw91VHoPsnKEu3nGSib0MAYFHCuCpZKlNqR40GdeIVzXfcX6Zcj2ifB3SjjGdMCBUtn_5GW9IfyY6Y9mWpfF9g-ajxoATc6ltNUe6PtbXk4nLUayzhsdF6hpAbvhxLd/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3o793dV8VX3E7JTw91VHoPsnKEu3nGSib0MAYFHCuCpZKlNqR40GdeIVzXfcX6Zcj2ifB3SjjGdMCBUtn_5GW9IfyY6Y9mWpfF9g-ajxoATc6ltNUe6PtbXk4nLUayzhsdF6hpAbvhxLd/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/dkt-godwin-mollell-wataalam-chukueni.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/dkt-godwin-mollell-wataalam-chukueni.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy