Serikali Haitawavumilia Wawekezaji Wanaochukua Mikopo Ya Magumashi-Waziri Mkenda
HomeHabari

Serikali Haitawavumilia Wawekezaji Wanaochukua Mikopo Ya Magumashi-Waziri Mkenda

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali haitawavumilia wawekezaji waliochukua...

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo June 8
Bajeti ya trilioni 14.94 Wizara ya fedha yapita
Mawakili waomba Sabaya akatibiwe uvimbe kichwani


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali haitawavumilia wawekezaji waliochukua mikopo ya kimagumashi na kutelekeza mashamba 16 ya maua na mboga mboga wilayani Arumeru Mkoani Arusha.


Waziri Mkenda ameyasema hayo jana tarehe 12 Juni 2021 wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo alipotembelea na kukagua mashamba yenye ukubwa wa Hekari 1950 wilayani Arumeru huku akiongeza kuwa wawekezaji hao walichukua mikopo lakini wameshindwa kurejesha mikopo hiyo na kuisababishia serikali hasara tangu mwaka 2018.


Waziri Mkenda amesema kuwa Mashamba hayo kwa mwaka mmoja yanapoteza zaidi ya fedha za kigeni Dola za Kimarekani Milioni 24 Sawa na ajira 6700 kwa mwaka.


"Serikali itahakikisha mashamba hayo yanarudi katika hali yake ya uzalishaji huku taratibu nyingine za kurejesha mikopo hiyo ikiendelea" Amekaririwa Prof. Mkenda na kuongeza kuwa


"Mashamba haya ya maua yamefungwa kutokana na wawekezaji waliochukua mikopo ya kimagumashi, mashamba haya yametelekezwa na yanaharibika wakati nchi hii tunahitaji fedha za kigeni na ajira kwa wananchi wetu, hivyo hatutamvumilia wala kumtetea aliyechukua mkopo kimagumashi" Amesema Prof. Mkenda


Prof. Mkenda ameongeza kuwa ni vigumu kuamini kampuni ambayo ilikuwa ikifanya biashara vizuri ingepewa mkopo halali na kuchukua mkopo wote hatimaye wakashindwa kuendeleza mashamba hayo. "Lazima kuna mchezo ulifanyika baina ya aliyetoa mkopo na aliyepokea mkopo ," Amesema Profesa Mkenda


"Wizara tunaenda kujenga hoja ili haya mashamba yaliyotelekezwa yanarudi katika hali yake ya kawaida ya uzalishaji na kama kuna wawekezaji wengine tuwape wayaendeleze ," Amesema Prof. Mkenda


Akizungumzia mashamba hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi Kilele ya mazao ya maua na mboga mboga (TAHA), Dkt. Jacqueline Mkindi amesema kuwa utelekezwaji wa mashamba hayo yamepoteza zaidi ya ajira 6700 za Watanzania na kuisababishia Serikali hasara kubwa ya kimapato.


Dkt. Mkindi ameeleza kuwa mashamba hayo yalikuwa yakiuza maua na bidhaa nyingine kwenye masoko ya Kimataifa na kuiomba Serikali kuona namna ya kuyarejesha kufanya kazi mashamba hayo ili yaweze kuongeza pato la Taifa na ajira kwa vijana na Watanzania kwa ujumla.


"Tunamshukuru Waziri kutembelea haya mashamba ambayo yametelekezwa, haya mashamba yalikuwa yanatoa maua ambayo yalikuwa takiuzwa kwenye masoko ya Kimataifa hivyo kufungwa kwa mashamba haya tumepoteza ajira takribani 6700 na kwa mwaka mzima tumepoteza fedha za kigeni wastani wa dola za Kimarekani sh. milioni 24 " Amesema Dkt. Mkindi


Aidha, Dkt. Mkindi aliongeza kuwa "Tunatamani siku moja kuona haya mashamba yanarudi katika uzalishaji na tuko tayari kutoa ushirikiano kwa serikali kuona ni namna gani ya kufufua haya mashamba na kutoa ajira kwa Watanzania," 


MWISHO



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Haitawavumilia Wawekezaji Wanaochukua Mikopo Ya Magumashi-Waziri Mkenda
Serikali Haitawavumilia Wawekezaji Wanaochukua Mikopo Ya Magumashi-Waziri Mkenda
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpR8bs7dj90PLZ7N7xHFkbLCTNX3v0M_oWnEdyi9ATaOrnX9ZH1adKVuzldp2wEfrCpVGROZwC8xnK7pb94kLX9zkymJQayz1FkP7a-pfrkZs7mwxO6J_YIkvOQBxBvgWO_tqdxufXgH7E/s16000/_KTC1090.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpR8bs7dj90PLZ7N7xHFkbLCTNX3v0M_oWnEdyi9ATaOrnX9ZH1adKVuzldp2wEfrCpVGROZwC8xnK7pb94kLX9zkymJQayz1FkP7a-pfrkZs7mwxO6J_YIkvOQBxBvgWO_tqdxufXgH7E/s72-c/_KTC1090.JPG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/serikali-haitawavumilia-wawekezaji.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/serikali-haitawavumilia-wawekezaji.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy