Serikali Kusitisha Vibali Vya Uagizaji Wa Sukari Ifikapo 2022-Waziri Mkenda
HomeHabari

Serikali Kusitisha Vibali Vya Uagizaji Wa Sukari Ifikapo 2022-Waziri Mkenda

 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Serikali imesema ifikapo Mwaka 2022 itasitisha utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nch...

Kenya yachukua urais wa Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa- UNSC
Waziri Gwajima Ashiriki Uzinduzi Wa Kituo Cha Udhibiti Wa Magonjwa Nchini Kenya
Vyama Vya Siasa Kuheshimu Sheria Na Maadili Ya Nchi Yetu


 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imesema ifikapo Mwaka 2022 itasitisha utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi kwa makampuni ambayo ndio wazalishaji wa ndani wa bidhaa hiyo.

Upungufu wa bidhaa hiyo nchini hautokani na uhaba wa miwa bali unasababishwa na makampuni kushindwa kuongeza uchakataji wa miwa kutoka kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo jana tarehe 5 Agosti 2021 katika ukumbi wa Asante Estates uliopo katika eneo la Ntyuka Jijini Dodoma aliposhiriki katika kongamano la saba la wadau wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo nchini.

“Baada ya mwaka huu Serikali haitotoa vibali kwa wawekezaji waliopewa viwanda vya sukari kuagiza sukari nje kwani tayari watakuwa wamefikia uwezo wa kuzalisha sukari toshelevu ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa uanzishwaji wa viwanda vipya vya sukari hapa nchini”

Waziri Mkenda amesema kuwa zaidi ya Tani 350,000 za miwa ya wakulima katika Bonde la Kilombero mkoani Morogoro zinateketezwa kwa moto kutokana na kukosa soko la uhakika lakini viwanda haviongezi uwezo wa kuchakata miwa ili kuzalisha sukari ya kutosha.

Amesema kuwa zaidi ya Tani 40,000 zinaagizwa kutoka nje ya nchi jambo ambalo sio sahihi kwani viwanda vya sukari vilivyopo nchini vinapaswa kuongeza uwezo wao ili kuimarisha soko la wakulima jambo litakalopelekea nchi kutoagiza sukari.

Waziri Mkenda amesema kuwa mtu yeyote atakayeingiza sukari kiholela ni wasaliti wa nchi hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kuwa kuna wimbi kubwa la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana lakini viwanda vimeshindwa kuongeza uwezo wake wa kuzalisha sukari ili kuimarisha sekta ya ajira kwa wananchi.

Katika mkutano huo Waziri Mkenda ameipongeza serikali na mawaziri waliotangulia kuiongoza Wizara ya Kilimo kwa kusimamia vyema sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kufanikisha kupunguza wimbi kubwa la uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Kusitisha Vibali Vya Uagizaji Wa Sukari Ifikapo 2022-Waziri Mkenda
Serikali Kusitisha Vibali Vya Uagizaji Wa Sukari Ifikapo 2022-Waziri Mkenda
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyJE5GbXnxNsC0ZPvjLLotuR5AmP-16ZCWsGCigWZwZOCZQ98EcYwbaB8QEPauCtt9ckHO1NmiMxg52yNXX0qbdOSLzzu_XT27_QNVZ1KDQrfYxJYSB-q0qNmy1TmKUQsJZ4hYr__aC8Uv/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyJE5GbXnxNsC0ZPvjLLotuR5AmP-16ZCWsGCigWZwZOCZQ98EcYwbaB8QEPauCtt9ckHO1NmiMxg52yNXX0qbdOSLzzu_XT27_QNVZ1KDQrfYxJYSB-q0qNmy1TmKUQsJZ4hYr__aC8Uv/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/serikali-kusitisha-vibali-vya-uagizaji.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/serikali-kusitisha-vibali-vya-uagizaji.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy