ISHU YA MAKAMBO NA YANGA IMEFIKIA HAPA
HomeMichezo

ISHU YA MAKAMBO NA YANGA IMEFIKIA HAPA

  D ILI la usajili wa  mshambuliaji  wa Horoya AC  ya Guinea, Her itier Makambo  limekamilika kwa asilimia  70 na kilichobakia ni kwa  mab...

YANGA: TUNAAMINI YALIYOFANYWA NA MAGUFULI YATAENDELEA KUTENDEKA ILI KUMUENZI
WAARABU KUWACHOMOA NYOTA HAWA WAWILI WA KIKOSI CHA KWANZA SIMBA
MBELGIJI WA SIMBA AMLILIA MAGUFULI

 DILI la usajili wa mshambuliaji wa Horoya AC ya Guinea, Heritier Makambo limekamilika kwa asilimia 70 na kilichobakia ni kwa mabosi wa GSM kuifuata timu yake hiyo kwa ajili ya kufikia muafaka.

 

Makambo ni kati ya wachezaji waliokuwa kwenye mipango ya kusajiliwa na Yanga katika usajili wa msimu ujao katika kuisuka safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

 

Hii siyo mara ya kwanza kwa Yanga kupanga kumrejesha mshambuliaji huyo kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo aliyeondoka msimu wa 2018/2019.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, mshambuliaji huyo amekubali kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakisha kwa sharti la mabosi hao kumfuata kwa ajili ya mazungumzo yatakayofikia muafaka mzuri.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa ni ngumu kwa Makambo kuandika barua ya kuondoka kwa uongozi wa Horoya kabla ya uongozi wa Yanga kumfuata kwa ajili ya mazungumzo.

 

Aliongeza kuwa mchezaji mwenyewe ameonyesha nia ya kutaka kuondoka Horoya baada ya kuona hapati nafasi ya kucheza katika kikosi hicho.

 

“Yapo mengi yanayoendelea kati ya Horoya na Makambo ambaye yeye amekubali kuandika barua kwa uongozi wa timu yake ya kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja ili aje ajiunge na Yanga katika msimu ujao.

 

“Makambo akiwa huko kocha wake anamtumia kucheza winga ambayo haitaki, yeye anataka kucheza namba 9 au 10 ambazo amekuwa akizicheza.

 

“Hivyo kitendo cha kukataa nafasi hiyo kimemfanya kocha wa Horoya kumuweka benchi, kwake kimeonekana kumkasirisha na kufikia hatua ya kutaka kuomba kuondoka hapa lakini anashindwa kutokana na kutopata timu, hivyo kama Yanga wakimfuata haraka ataandika barua ya kusitisha mkataba ili aondoke,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Championi Jumatano, lilimtafuta Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Wapo wachezaji wengi walio katika mipango yetu ambao ni siri, tumepanga kuwatambulisha mara  baada ya kumaliza taratibu zote za usajili.

 

Makambo mwenyewe hivi karibuni aliandika ujumbe kwenye mtandao wa jamii uliosomeka hivi: “Nimewamisi Yanga, nimewamisi mashabiki wa Yanga.”



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: ISHU YA MAKAMBO NA YANGA IMEFIKIA HAPA
ISHU YA MAKAMBO NA YANGA IMEFIKIA HAPA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBj1ZbRQVx2XnbeETNOu8OnKNiQN_cq-VKv5RClYn-par8nMsth76ZmgmrPfG3KFvYr3TG3E4sQ56N3I_ATN6Do-A1fY-pTX7rJ2-WXMhXv-qfEm8u0N6u1VTFhl_haJ0U300GYEs5Wy4J/w640-h426/Makambo.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBj1ZbRQVx2XnbeETNOu8OnKNiQN_cq-VKv5RClYn-par8nMsth76ZmgmrPfG3KFvYr3TG3E4sQ56N3I_ATN6Do-A1fY-pTX7rJ2-WXMhXv-qfEm8u0N6u1VTFhl_haJ0U300GYEs5Wy4J/s72-w640-c-h426/Makambo.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/ishu-ya-makambo-na-yanga-imefikia-hapa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/ishu-ya-makambo-na-yanga-imefikia-hapa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy