UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utawafuata wapinzani wao JKT Tanzania kwa tahadhari kubwa huku wakihitaji ushindi kupata pointi tatu m...
UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utawafuata wapinzani wao JKT Tanzania kwa tahadhari kubwa huku wakihitaji ushindi kupata pointi tatu muhimu.
Mei 15, Uwanja wa Majaliwa ubao ukisoma Namungo FC 0-0 Yanga uliwafanya mashabiki na wachezaji kupoteza furaha kwa sababu walifutiwa bao lao jambo lililowafanya wagawane pointi mojamoja.
Leo Mei 17 kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuanza safari kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Mei 19.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro amesema kuwa wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS