WAZIRI NDUMBARO AZITAKA WIZARA KUSHIRIKI MAJIMAJI SELEBUKA
HomeMichezo

WAZIRI NDUMBARO AZITAKA WIZARA KUSHIRIKI MAJIMAJI SELEBUKA

WAZIRI wa Maliasili  na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zote za Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zinatangaza Utalii na z...

SIMBA YATAJA SABABU YA NYOTA WATANO KUBAKI BONGO
PIRA KODI LEO KUCHEZWA MBELE YA POLISI TANZANIA
DITRAM NCHIMBI, ADEYUM KUIKOSA COASTAL UNION LEO MKWAKWANI

WAZIRI wa Maliasili  na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zote za Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zinatangaza Utalii na zinafanya Uhifadhi kuweza kushiriki Tamasha la Majimaji Selebuka.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma  kuanzia 24 Julai hadi 31 mwaka huu katika Uwanja wa Majimaji Songea likiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani, michezo pamoja na kukuza na kuenzi utamaduni.


Ametoa agizo  hilo wakati  akizindua msimu wa saba wa Tamasha hilo uliofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia 24 na 25 Aprili katika Viwanja vya Makumbusho ya Majimaji  ikiwa ni maandalizi ya Tamasha lenyewe litakalofanyika mwezi Julai  kwa muda wa siku saba mkoani hapo.



Katika Tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo " Misitu ni Uchumi " Dkt.Ndumbaro amesema kwa mwaka huu Tamasha linatoa hamasa kwa  Jamii  kutunza misitu zaidi.


 Ndumbaro amesema anategemea tamasha hilo kwa mwaka huu litakuwa kubwa sana na litatoa fursa kwa Watu mbalimbali  kuanza kutembelea  vivutio mbalimbali vya Utalii ambavyo vipo mkoani Ruvuma likiwemo Pori la Akiba Lipalamba.

Katika hatua nyingine, amemuomba mkuu wa  wilaya ya Songea  kutumia mamlaka yake ya kuzitaka Taasisi zilizo katika wilaya yake kushiriki katika tamasha hilo.

" Mkuu wa wilaya najua una taasisi nyingi sana katika wilaya yako ninakuomba na ninaamini una mamlaka hiyo, toa maelekzo kwa taasisi zote zinanazotoa huduma na kufanya biashara zishiriki tamasha la Majimaji Selebuka " alisisitiza Ndumbaro. 


Aidha amezitaka Halmashauri ya Songea pamoja Halmashauri zingine ziweze kushiriki tamasha hilo na   ametumia fursa hiyo kuziomba taasisi nyingine za watu binafsi kushiriki katika tamasha hilo ili ziweze kutoa huduma kwa jamii katika msimu wa tamasha hilo.


Kwa upande wake Mratibu wa tamasha hilo Reinfrida Rwezaura, amesema tamasha hilo tangu kuanzishwa kwake limekuwa ni jukwaa bora kwa kuwakutanisha Wafanyabiashara, Wajasiliamali, Wanamichezo, Wanafunzi, na Wadau mbalimbali katika kuendelea kuutangaza uchumi na utalii nchini. 




Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: WAZIRI NDUMBARO AZITAKA WIZARA KUSHIRIKI MAJIMAJI SELEBUKA
WAZIRI NDUMBARO AZITAKA WIZARA KUSHIRIKI MAJIMAJI SELEBUKA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_vFauWKxsZJssYXwPNbz4u4jRFr-f6ia_TwWOlgQsFV8-CoY9biecwpNYYhxCkUYZ-LogpDXcOXCoWsRr6aSHNDn3dD56SzmZPA1YqhBA4pF_qA03Qr3WzB55qFQ6jmUxEV57G9eeIJml/w640-h426/1+%25285%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_vFauWKxsZJssYXwPNbz4u4jRFr-f6ia_TwWOlgQsFV8-CoY9biecwpNYYhxCkUYZ-LogpDXcOXCoWsRr6aSHNDn3dD56SzmZPA1YqhBA4pF_qA03Qr3WzB55qFQ6jmUxEV57G9eeIJml/s72-w640-c-h426/1+%25285%2529.JPG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/waziri-ndumbaro-azitaka-wizara.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/waziri-ndumbaro-azitaka-wizara.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy